Tangu mwaka 2015 umeanza tumesikia stori kadhaa za Ajali ya moto ikiwemo
ile ya familia yenye watu sita wakiwa wamefariki ndani ya
nyumbani chanzo kilisemakana ni itilafu ya Umeme,
sasa hapa nakusogezea stori nyingine ya kusikitisha ambapo usiku wa
kuamkia leo kumetokea ajali ya moto ilyouwa familia ya watu 9 wakiwa
ndani ya nyumba maeneo Buguruni Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu wa mtaa Amina Kichalala….’Mimi
niliamshwa usiku na mume wangu akatuambia kwa jirani kuna moto ilikuwa n
majira ya saa tisa usiku mara tunasikia sauti zao wanasema tuwasaidie
moto ulikuwa ni mkubwa sana watu wakaanza kurusha mawe, wamejitahidi
lakini moto ukawa mkubwa mpaka mida ya saa kumi na moja kasoro ndio
zijaka fire kuuzima huo moto na kutoa miili ya watu tisa wakiwa
washamefariki katika ajali hiyo ya moto’ – Amina
‘Sauti
iliyosikika wakati tukio hilo la ajali ya moto ilikuwa ni ya msichana
mdogo anaitwa Aisha yuko kama darasa la saba motto wa huyo Baba, katika
hiyo nyumba alikuwa anaishi Mama Habilai, Mohamed, Ashlafu,Aisha na Bibi
yao asiyejiweza kwasababu uwa wanamtoa kumpeleka hospitali na wageni
kutoka Oman walioingia jana nao wamefariki’ – Amina
‘Majirani
walifanya juhudi za kuuzima moto huo lakini hakuna kilichowezekana
kwasababu moto ulikuwa ni mkubwa sana, uamuzi uliofuata ile miili 9 ya
ndugu zetu imepelekwa muhimbili kuoshwa na kuzikwa katika makaburi ya
Kisutu Dar es Salaam‘ -Amina
0 comments:
Chapisha Maoni