Rais Jakaya Kikwete ameendelea kuthibitisha kuwa ni mtetezi namba moja wa maslahi ya wasanii wa Tanzania baada ya jana kuwahakikishia mustakabali wa kuvutia.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na wasanii wa muziki na filamu jana Mlimani City
Akiongea mbele ya wasanii kwenye hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na kile kilichoitwa ‘muungano wa wasanii wa Tanzania’ kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Kikwete alisema angependa kuona wasanii wanapata mafanikio kama wanayopata wale wa nchi zilizoendelea.
P-Funk Majani na Matonya
“Akina Beyonce wale pamoja na umri mdogo, akina Chris Brown pamoja na uhuni, na mpenzi wake Rihanna, pamoja na machachari yao yote lakini ni matajiri sana,” alisema Kikwete.
Diamond Platnumz akisema machache
“Na ni kwasababu ni matajiri sana wana pesa nyingi katika umri mdogo kila wanachokihitaji katika maisha wamemaliza, wanaenda kufanya hata mambo ambayo hayana maana, kwasababu wametajirika. Akina Brad Pitt, George Clooney ni matajiri wanalipwa malipo ya haki kwa kazi halali. Sisi wasanii wetu wananufaika watu wa kati. Alipokufa Kanumba pamoja na umaarufu wote hana kazi yoyote ipo kwa jina lake. Kwamba Kanumba amekufa lakini kazi zote alizozifanya ni mali ya watu wa kati,” alisisitiza.
Madam Rita na Natasha wakibadilisha mawili matatu
Rais Kikwete alidai kuwa hawezi kukubali kuona hali hiyo inaendelea na kwamba serikali itaingilia kati.
Ruby akitumbuiza jana mbele ya Rais Kikwete na watu wengine
Katika hatua nyingine Rais Kikwete aliwapa agizo COSOTA kuhakikisha kuwa wasanii wanaanza kulipwa mirahaba kupitia kuchezwa kwa kazi zao kwenye vituo vya redio na TV.
Rais Kikwete akisalimiana na meneja wa Diamond, Sallam, katikati ni Diamond
Shilole na Baby J
Alikiba (katikati) akiwa na timu yake
0 comments:
Chapisha Maoni