Rais
Kikwete, mgombea Urais Dk. MAGUFULI, LOWASSA pamoja na Freeman Mbowe
wanatarajia kukutana katika mazishi ya muasisi wa TANU na CCM marehemy
Peter Kisumo.Lowassa ni mgombea Urais Chadema mbaye atapeperusha bendera
kupitia umoja wa katiba ya wananchi UKAWA akishindana na Magufuli
aliyeteuliwa na vikao vya juu vya CCM kuwa mgombea wake wa Urais licha
kuwepo manung’uniko kuwa uteuzi wake haukufuata utaratibu.
Taarifa zinasema wanasiasa hao watahudhuria mazishi hayo yaliyopangwa kufanyika Augusti 13 Mkoani Kilimanjaro.
Rais
Kikwete ndiye anayetarajiwa kuwaongoza wakazi wa Kilimanjaro katika
mazishi hayo ya aliyekuwa mwasisi wa TANU na baadaye CCM.
MWANANCHI
Rais Jakaya Kikwete amesema sasa atazungumza lugha moja na wakwe zake baada ya kukamilika Barabara ya Ndundu-Somanga kwa kiwango cha lami.
Rais
Kikwete alisema hayo juzi jioni kwenye sherehe za ufunguzi wa barabara
hiyo iliyofanyika Kijiji cha Marendego Mpakani na kuhudhuriwa na
wananchi wa mikoa ya Lindi, Pwani pamoja na viongozi mbalimbali wa chama
na Serikali akiwamo Balozi wa Kuwait nchini, Jassem Ibrahim AL- Najem.
“Nimekuwa
mwenye furaha sana maana barabara hii ilikuwa ikininyima usingizi kwa
sababu mbili; kwanza kuchelewa kumalizika na vilevile kile kilio cha
kuhitaji hii barabara ilikua ni kilio cha muda mrefu sana cha wananchi
wa mikoa hii ya kusini cha wabunge wao na viongozi wao.
“Lakini
siyo hilo pekee, kwa sisi tuliooa mikoa ya huku, imenipa tabu pia, kila
wakati naulizwa mbona humalizi barabara ya kwetu, ninasema itaisha, kwa
hiyo nafurahi leo ndugu Magufuli (John) umeniondolea unyonge,
ninasimama hapa kwa kujiamini. Wakwe zangu na shemeji zangu ugomvi sasa
umeisha, kwa hiyo nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitakushukuru Waziri
Magufuli. kwa kuwa mstari mbele kusimamia ujenzi huu na hata katika
maeneo mengine umekuwa mtendaji wa kuigwa,” Kikwete
Akitoa
taarifa ya barabara hiyo Dk Magufuli alisema sehemu hiyo ya kilomita 60
ndiyo iliyokua sehemu pekee iliyobaki kujengwa kwa kiwango cha lami,
mradi huo umegharimu Sh77.2bil na kutekelezwa kwa kugharamiwa na
Serikali ya Tanzania kwa asilimia 55, Mfuko wa Kuwait kwa asilimia 31 na
mfuko wa OPEC kwa asilimia 14.
Naye Balozi AL-Najem alisema kwamba ziara ya Rais Kiwete nchini humo ndiyo chimbuko ya mafanikio ya barabara hiyo.
Mapema mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa
salamu za mkoa alisema awali usafiri wa wananchi kutoka Ndundu
ilichukua siku mbili hadi tatu kwenda mikoa ya Lindi na Mtwara au kutoka
kwenye mikoa hiyo kuja Pwani na Dar esaaam kutokana na eneo hilo kuwa
mbaya na hivyo magari mengi yalikuwa yanakwama kuendelea na safari
yakifika hapo lakini sasa safari ni kwa saa,” alisema.
MWANANCHI
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambaye alianguka katika hatua za awali za mbio za urais ndani ya CCM, amesema ameishia kuwa “rais wa fikra”.
Pinda,
ambaye amekuwa Waziri Mkuu kwa takriban miaka minane, hakuweza kuingia
katika orodha ya makada watano ambao majina yao yalipelekwa Halmashauri
Kuu kwa ajili ya kupata majina matatu ya kupelekwa Mkutano Mkuu kwa
ajili ya kupata mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho tawala.
Baada
ya mchakato huo kumalizika, mbunge huyo wa Katavi amekuwa kimya, lakini
jana aliibuka na kuzungumzia mbio hizo zilizoacha majeraha kwenye chama
hicho kikongwe.
Pinda
alisema mchakato huo ulikuwa hauna kulala, wa haraka haraka, ambao
uliisha kwa CCM kupata mgombea ambaye alimuelezea kuwa “ni chaguo la
Mungu”.
Akizungumza
baada ya kupokea taarifa fupi ya Mkoa wa Mbeya kuhitimisha maonyesho ya
Nanenane jijini hapa, Pinda alisema alitamani sana kuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano Tanzania.
“Mimi
ninaamini Mungu ndiye anayepanga kwani sikuzaliwa kuwa Waziri Mkuu
wala kuwa Rais, lakini nilipangiwa uwaziri mkuu ambao nimefanya kazi
hiyo hadi nimechoka,” alisema Pinda, ambaye alikuwa mmoja wa makada 42 wa CCM waliojitokeza kuwania ridhaa ya chama hicho kugombea urais.
“Baada ya mchakato ule, alipatikana mtu mahiri ambaye Mungu alimpanga, lakini tamaa yangu, ikaishia kuwa rais wa fikra tu.”
Alisema mchakato ulifanyika kwa kasi bila kulala na wakapatikana watano, mara watatu na hatimaye mmoja.
“Suala
hilo halitakiwi kuwa sababu ya kugombana, kulaumiana na kutoana macho,
kwani ni sawa na kugombana na Mungu,” alisema Pinda.
“Hata
mimi nilitamani sana kuwa Rais, lakini sasa yamekwisha. Sina sababu ya
kuwa na hasira au kuhama chama kwani haina tija na hasira ni hasara.
“Sina
sababu ya kuhama chama, nitabaki CCM na baada ya Oktoba nitakuwa
mkulima mzuri ambaye nitashirikiana na wenzangu kuendeleza nchi.” Pinda
alisema mgombea wa CCM, Dk John Magufuli ni mzuri na kwamba Mungu
atamsaidia kujua mahitaji mengine ya Taifa na Watanzania.
Alisema ana uhakika kwamba ifikapo mwaka 2025, hali ya umaskini katika kaya itakuwa imepungua.
Aliwataka
wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na maofisa wote wa Serikali waliogombea
urais, ubunge na udiwani ambao walishindwa katika kura mbalimbali,
wakubali matokeo na wachape kazi bila kinyongo na kwamba Serikali ijayo
itawafikiria kwa utendaji mzuri.
MWANANCHI
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kesho
atachukua fomu za kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wakati msafara wake utakapoanzia ofisi za makao makuu ya CUF kuelekea
ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na baadaye kwenda kumalizia
makao makuu ya Chadema yaliyoko Kinondoni.
Safari
ya Lowassa, ambaye anawania urais kwa tiketi ya Chadema na chini ya
mwamvuli wa vyama vinne vya CUF, NCCR-Mageuzi, Chadema na NLD, itakuwa
ya umbali wa kilomita 11, ikihusisha wilaya mbili za Ilala na Kinondoni.
“Yeyote anayejisikia kutaka kumsindikiza Lowassa, anakaribishwa,” alisema kaimu katibu mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu jana alipozungumza na waandishi wa habari.
“Tutaanzia CUF na kumalizia Chadema. (Lowassa) ataambatana na mgombea mwenza, Juma Duni Haji.”
Kwa
mujibu wa Mwalimu, msafara huo utaanzia ofisi hizo za CUF zilizoko
Buguruni na kwenda katikati ya jiji, takriban kilomita tano, ambako
Lowassa atachukua fomu ofisi hizo za NEC na baada ya tukio hilo, msafara
utakwenda Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, takriban kilomita sita, ambako ni
makao makuu ya chama hicho kikuu cha upinzani.
Lowassa,
ambaye alibadili upepo wa mbio za urais baada ya kuihama CCM na
kujiunga na Chadema iliyompa fursa ya kuwania nafasi hiyo, atakuwa mtu
wa saba kuchukua fomu hizo tayari kwa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika
Oktoba 25.
Wengine waliochukua fomu hizo ni John Magufuli wa CCM, Mchungaji Christopher Mtikila (DP), Chifu Lutayosa Chemba (ADC), Macmillan Limo (TLP), Hashimu Rungwe (Chauma), Fahami Dovutwa (UPDP) na Dk Godfrey Malisa (CCK).
Akiongea
na waandishi wa habari makao makuu ya NCCR jana, Mwalimu alisema
msafara wa kumsindikiza Lowassa utaanzia saa 3:00 asubuhi.
Alisema
mara baada ya kukamilisha kazi ya uchukuaji fomu, kuanzia Agosti 14,
Lowassa ataanza ziara katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kutafuta
wadhamini, ikiwa ni baada ya kushiriki mazishi ya kada mkongwe wa CCM,
Peter Kisumo yatakayofanyika Agosti 13, mkoani Kilimanjaro.
“Hatakwenda
mikoa yote kutokana na muda, lakini tatizo jingine kila mwanachama
anataka mgombea wetu (Lowassa) aende mkoa aliopo. Hili limetupa tabu na
ndiyo sababu ya kubadilika kwa ratiba zetu,” alisema.
“Tutaeleza ratiba kamili na katika mikoa ambayo Lowassa hatafika kwa sasa, atafika wakati wa kampeni,” alisema Mwalimu.
Kuhusu ugawaji wa majimbo, Mwalimu alisema kazi hiyo imeshafanyika na siku yoyote kuanzia leo watatangaza.
“Tumeyagawa
majimbo yote yakiwemo yale 26 mapya kwa kuzingatia umoja wetu wa Ukawa.
Najua siku zimebaki chache kabla ya uchaguzi mkuu, hivyo tutatangaza tu
kuanzia kesho (leo),” alisema.
MWANANCHI
CCM
imesema haitarudia makosa ya mwaka 2010 ya kutengua uamuzi wa
wanachama, lakini itahitaji kuwa na moyo mgumu baada ya makada wengi
kukata rufaa kupinga matokeo ya kura za maoni.
CCM
inamalizia hatua ya mwisho ya mchakato wake wa ndani wa kupata wagombea
ubunge na udiwani kwa vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu
vitakavyopitia majina ya makada wote walioshinda kwenye kura za maoni,
ambazo zilitawaliwa na tuhuma za rushwa na ukiukwaji wa taratibu.
Vikao
hivyo huwa vinaweza kutengua ushindi wa kada kwenye kura za maoni kwa
kuangalia rufani zinazopinga mchakato, tuhuma za rushwa na ukiukwaji wa
taratibu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema wamepokea malalamiko mengi kuhusu ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi katika upigaji wa kura za maoni.
“Kumekuwa
na utamaduni wa kulalamika barabarani wakati mwingine kushawishi
wanachama kulalamika kwenye vyombo vya habari na kwingineko. Utaratibu
huu si wa chama chetu,”Nape.
“Tunashauri taratibu zifuatwe. Katika kufikia hatua hii tunawaomba wanachama wawe watulivu.”
Alisema
wanachama wamejaa mjini Dodoma wakijaribu kushawishi wajumbe kuhusu
rufaa zao, lakini akasema kinachotakiwa kiwasilishwe ni malalamiko yao,
ushahidi wa kutosha katika ngazi husika.”
Nape
pia alisema kumezuka wimbi la matapeli linalowalaghai makada
walioshindwa katika kura za maoni kuwa watoe fedha ili wawasaidie rufaa
zao kwenye vikao hivyo.
Alisema
matapeli hao wamesajili namba za simu za viongozi wa CCM na kwamba yeye
ni mmoja wa viongozi walioathirika na utapeli huo kwa namba yake ya
simu ya mkononi kutumika.
MWANANCHI
Mjumbe wa Iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole amesema
yupo tayari kufanya kampeni za kumpinga mgombea urais wa Chadema na
Ukawa, Edward Lowassa kwa madai kuwa ana doa linalomzuia kuwania nafasi
hiyo.
Polepole
ameibuka kuwa maarufu tangu kumalizika kwa Bunge la Katiba, akishiriki
kwenye midahalo kadhaa kuhusu mchakato wa kuandika Katiba mpya,
akitofautiana na msimamo wa CCM wa kubadilisha Rasimu ya Katiba.
Akizungumza
na Mwananchi jana, Polepole alisema Lowassa anayeungwa mkono na vyama
vya NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), ana tuhuma za ufisadi na ni mmoja wa makada wa CCM
walioipinga Rasimu ya Katiba.
Polepole
alisema msingi wa kuzaliwa kwa Ukawa ni kutaka Katiba mpya yenye maoni
ya wananchi, hivyo Chadema kumpokea Lowassa ni sawa na kukiuka misingi
hiyo.
“Nimeshirikiana
na Ukawa na viongozi wao kama Watanzania kuhakikisha Taifa letu
linapata Katiba mpya na inayotokana na maoni ya wananchi. CCM ambao
walikuwa ndiyo wana mkakati na wenye maamuzi ya mwisho katika kukwamisha
maoni ya wananchi. Watu hao (wa CCM) hawastahili kupewa uongozi iwe
ndani ya CCM au hata ndani ya Ukawa,” alisema.
embu soma na hii, inakuhusu ukawa
Nape Nnauye Awatuhumu UKAWA Kwa Kutengeneza Kadi Bandia za CCM
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi wa
CCM, Nape Nnauye, amedai kuwa chama hicho kimebaini mchezo mchafu
unaotaka kufanywa na Ukawa wa kutengeneza kadi bandia za chama hicho na
kuzigawa kwa watu wao, ili baadaye asipopita mgombea wao, ionekane wana
CCM wanakihama chama kwa kurudisha kadi zao.
Akizungumza katika Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma jana, Nape alisema kuna taarifa za uhakika kuwa kuna baadhi ya makundi ya Ukawa yamepanga mchezo huo wa kutengeza kadi bandia.
“Wameanza kuratibu mchezo huo ili wazigawe kadi hizo kwa watu wao, ili baadaye asipopita mgombea wao, ionekane wana CCM wanakihama chama chao kwa kurudisha kadi hizo kwenye shughuli mbalimbali za vyama hivyo vinavyounda Ukawa.
“Wakati tunachunguza kwa kina suala hilo, Ukawa waache mchezo huo wa ovyo na Watanzania wakwepe mchezo huo na wawe makini,” alisema
Akizungumza katika Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma jana, Nape alisema kuna taarifa za uhakika kuwa kuna baadhi ya makundi ya Ukawa yamepanga mchezo huo wa kutengeza kadi bandia.
“Wameanza kuratibu mchezo huo ili wazigawe kadi hizo kwa watu wao, ili baadaye asipopita mgombea wao, ionekane wana CCM wanakihama chama chao kwa kurudisha kadi hizo kwenye shughuli mbalimbali za vyama hivyo vinavyounda Ukawa.
“Wakati tunachunguza kwa kina suala hilo, Ukawa waache mchezo huo wa ovyo na Watanzania wakwepe mchezo huo na wawe makini,” alisema
0 comments:
Chapisha Maoni