Katibu wa Mipango na Mikakati wa ACT – Wazalendo, Habibu
Mchange aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba maandalizi ya
uzinduzi huo yanaendelea vyema na kwamba hafla hiyo itahudhuriwa na
viongozi wote wa kitaifa wa chama hicho wakiwamo Kiongozi wa Chama,
Zitto Kabwe na Mwenyekiti wake, Anna Mghwira ambaye pia ni mgombea
urais.
“Baada ya mwenyekiti wetu, Mama Mghwira kuchukua fomu ya kugombea
urais, Watanzania wamekuwa na shauku ya kutaka kujua mustakabali wetu
kuelekea Uchaguzi Mkuu,” alisema na kuongeza: “Hivyo basi
tunawakaribisha wananchi wote siku hiyo waje kushuhudia kampeni za
kisayansi. Ndiyo maana tumeamua kuwaita wagombea ubunge wote kuhudhuria
na kuwatambulisha rasmi kwa Watanzania.”
Alisema ACT – Wazalendo imejipanga kuchukua dola na kuleta siasa
safi, tofauti na vyama vingine akisisitiza kuwa kina nia ya dhati ya
kuwaletea maendeleo ya Watanzania. Hivyo kuwataka wananchi kuhudhuria.
Alisema katika siku ya uzinduzi, kwa mara ya kwanza wabunge waliohama
kutoka vyama vya CCM, CUF na Chadema watazungumza, pia wataendelea
kuinadi ilani ya uchaguzi wa chama hicho. Alisisitiza kuinadi kaulimbiu
ya chama hicho ya utu, uadilifu na uzalendo.
Katibu wa Fedha na Rasilimali ya chama hicho, Peter Mwambuja alisema
pia kimejipanga kufanya siasa za malengo na masuala kwa maendeleo ya
Watanzania siyo kupiga propaganda.
0 comments:
Chapisha Maoni