Jeshi
la Polisi nchini kikosi cha usalama barabarni limetoa muda wa miezi
miwili kuanzia sasa kwa wamiliki wa vyombo vya moto kuhakikisha wanaweka
viakisi mwanga katika magari na kwamba hatua kali za kisheria zitaanza
kuchukuliwa kwa watakao kiuka agizo hilo.
Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na kikosi cha usalama barabarani
nchini imesema kuwa uwekaji wa viakisi mwanga hivyo kwenye magari
utasaidia kupunguza ajali zinazosababishwa na baadhi ya magari
yaliyoharibika njiani zoezi litakalo kuwa sambamba na uwekaji wa stika
kwenye magari.
Kwa muda sasa askari wa usalama barabarni wamekuwa wakilalamikiwa
kutokuva sare pindi wanapokagua mwendo kasi kwa magari ya mikoani,
lakini kamanda Mpinga anasema zoezi hilo litaendelea na kuwataka
madereva kutii na kuheshimu kanuni za barabarani.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
kamanda Mpinga ametumia fursa hiyo kupiga marufuku kwa watumiaji wa
vyombo vya moto ambao wamekuwa wakitumia barabara za mwendo kasi na
kwamba kuanzia jumatatu wiki hii adhabu kali za kisheria zitaanza
kuchukuliwa kwa watakao bainika.
0 comments:
Chapisha Maoni