Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amefunguka kwa mara ya kwanza na kuweka wazi kilichotokea mjini Dodoma na kusababisha ashindwe katika uteuzi wa kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Membe
amekuwa kada wa tatu kueleza hadharani jinsi uteuzi huo ulivyoendeshwa
ambao Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, aliibuka kidedea kati ya
makada 42 waliojitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa.
Makada
wengine waliojitokeza hadharani kuelezea mchakato huo ni Waziri Mkuu wa
zamani, Edward Lowassa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),
Prof. Mark Mwandosya, ambao kwa nyakati tofauti walieleza sababu
mbalimbali zilizosababisha kushindwa kwao.
Membe
akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika kongamano la pili la
Watanzania waishio ughaibuni (Diaspora), alisema mchakato huo ulikuwa ni
sawa na timu mbili za mpira wa miguu zilizokuwa zinapambana uwanjani.
Alisema unaweza ukapata timu nzuri sana ya mpira kwenye ligi na ikashinda michezo yote bila kufungwa goli hata moja.
Aliongeza
kuwa lakini mwishoni timu hiyo inapotoka sare na timu nyingine ambayo
ni dhaifu kwenye fainali, timu hizo zinakwenda kwenye penalti kwa kuwa
mshindi lazima apatikane.
Membe
alieleza kuwa wakati wa upigaji penalti timu hiyo ambayo ilitarajiwa
kuibuka na ushindi kwa kuwa ilicheza mpira safi ikafungwa penalti zote
tano na hiyo timu ambayo haikutegemewa ikashinda mabao yote.
Alisema
kuwa kwenye ‘football jargon’ kitendo hicho cha timu iliyocheza mpira
vizuri na kudhaniwa ingeibuka na ushindi, lakini ikashindwa kwenye
penalti, timu hiyo imekufa kifo cha ghafla.
Membe
aliendelea kueleza kuwa timu hiyo itakuwa imepigwa kifo cha ghafla na
kueleza kuwa inapopigwa kifo cha namna hiyo timu hiyo haiwezi kutegemewa
isimame na ielezee kilichotokea.
“Naomba
leo nitumie nafasi hii kwa mara ya kwanza kuelezea kilichotokea mjini
Dodoma katika uchaguzi wa nafasi ya urais kwa Chama Cha Mapinduzi na
nadhani sitaulizwa tena,” alisema Membe.
Mfano
huo huenda ukahusishwa na wanachama wa CCM waliokuwa wanamuunga mkono
Membe kama timu iliyokuwa inatumainiwa ingeshinda mchakato huo, huku Dk.
Magufuli akielezwa kama timu ambayo haikudhaniwa kushinda
kinyang’anyiro hicho kutokana na kutokuwa na makundi yaliyokuwa
yanamuunga mkono.
Membe alikuwa na kundi kubwa la wafuasi akimfuatia Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Lowassa
na Membe walikuwa miongoni mwa makada sita ambao walipewa adhabu ya
kufungiwa mwaka mmoja kuanzia Februari, mwaka jana hadi Mei, mwaka huu,
baada ya kubainika kuwa walianza kampeni mapema kabla ya wakati kinyume
cha kanuni za chama hicho
0 comments:
Chapisha Maoni