Skip to content
1. Wivu Wa Kupindukia
Ni Jambo Jema Kwa Mwanamume Kumtakia Heri
Mpenzi Wake Na Kufanya Kila Awezalo Kuhakikisha Kuwa Hapati Madhara,
Lakini Iwapo Utakuwa Mtu Wa Wasiwasi Na Mashaka Pale Unapomwona Mpenzi
Wako Akizungumza Na Mwanamume Mwingine, Au Anapotoka Na Marafiki Zake Wa
Kike, Au Anapovaa Nguo Inayomfanya Atamanishe, Basi Fahamu Kuwa Tayari Umekunywa Sumu Ya Mapenzi.
Katika Uhusiano Wa Kimapenzi,
Kuaminiana Ni Jambo Muhimu Sana. Kama Kweli Unataka Mpenzi Wako Akupende
Kwa Dhati, Mwoneshe Kuwa Unamwamini Na Unaheshimu Maamuzi Yake, Ikiwa
Ni Pamoja Na Maamuzi Ya Kutoka Na Marafiki Zake Wa Kike Na Kuwa Na
Marafiki Wa Kawaida Wa Kiume. Ondoa Hofu Na Acha Kabisa Kumpeleleza,
Maana Wapo Wanaume Ambao Hutumia Muda Wao Mwingi Kuwapeleleza Wapenzi
Wao Ikiwa Ni Pamoja Na Kuwategeshea Kamera Na Rekoda Za Simu.
2. Kutomwachia Nafasi Mpenzi
Kama Huishi Na Mpenzi Wako Ni Jambo La
Kawaida Kuwa Na Hamu Ya Kumwona Mara Kwa Mara, Lakini Kumbuka Kuwa
Mpenzi Wako Naye Ana Maisha Yake Na Anahitaji Nafasi Ya Kuwa Peke Yake
Kwa Ajili Ya Mambo Yake Binafsi.
Hisia Za Kutaka Kuwa Na Mpenzi Wako
Muda Wote Zinaweza Kudhaniwa Kuwa Ni Za Mapenzi Ya Dhati, Lakini Kwa
Hakika Hiyo Si Ishara Njema Ya Mapenzi Ya Kudumu. Hebu Jiulize Kama
Unaweza Kuendeleza Hali Hiyo Maisha Yako Yote. Ni Wazi Kuwa Utachoka.
Kwa Hiyo, Mpe Mpenzi Wako Fursa Ya Kupumua. Namna Hii Mpenzi Wako
Atajenga Hamu Ya Kutaka Kukutana Nawe Lakini Ukiwa Naye Muda Wote Hamu
Hiyo Itaisha.
3. Kumwamulia Mpenzi Mambo Yake
Unaweza Kujikuta Ukisukumwa Kumwambia
Mpenzi Wako Awe Anavaa Nini Wakati Gani, Akutane Na Nani Na Kwa Wakati
Gani Au Ale Nini. Ukiona Hivyo, Fahamu Kuwa Hayo Si Mapenzi, Bali
Umepitiliza Na Pengine Mwisho Wa Uhusiano Wenu Unanukia.
Hata Ukiachilia Mbali Suala Zima La
Usawa Wa Jinsia, Hakuna Mwanamke Ambaye Angependa Apangiwe Kila Kitu
Kuhusiana Na Maisha Yake. Kama Ilivyodokezwa Hapo Juu, Kila Mtu Ana
Maisha Yake Na Kilichowaunganisha Ni Mapenzi Tu. Kama Utataka Kumpangia
Kila Kitu Ni Wazi Kuwa Utaishia Kuishi Peke Yako.
4. Kumuuliza Mpenzi Maswali
Iwapo Utajikuta Ukimuuliza Mpenzi Wako
Maswali Mengi Yanayoonesha Wasiwasi Wako Kuhusiana Na Mwenendo Wake,
Fahamu Kuwa Kuna Tatizo Na Tatizo Hilo Lisipopatiwa Ufumbuzi Utakuwa
Mwanzo Wa Mwisho Wa Uhusiano Wenu.
Mwanamke Angependa Umuulize Maswali Ya
Kawaida Kuhusiana Na Jinsi Siku Yake Ilivyokuwa Na Kama Marafiki Zake
Hawajambo Au La, Lakini Kila Jambo Lina Mpaka Wake. Mwanamke Hatarajii
Kuwa Kila Mnapokutana Atakuwa Kama Ameingia Kwenye Chumba Cha Mtihani Au
Usaili Wa Kazi.
5. Kutoamini Anachokweleza Mpenzi
Wakati Mwingine Watu Hushindwa Kuwaamini
Wenzao, Lakini Kwa Sababu Ambazo Ni Za Msingi, Lakini Kuna Wakati Ambapo
Mtu Hushindwa Kumwamini Mwenzake Bila Sababu Yoyote Ya Msingi, Au Kwa
Sababu Zisizo Sahihi, Kisingizio Kikiwa Ni Mapenzi.
Kuna Tatizo La Kisaikolojia La
Kujishuku Au Kuwashuku Wenzako. Hili Ni Jambo Ambalo Linaweza
Kukuharibia Mustakabali Wako Katika Mapenzi, Maana Husababisha Kujengeka
Kwa Mazingira Ya Kutokuaminiana. Ili Uweze Kwenda Sanjari Na Mpenzi
Wako, Amini Kila Anachokweleza Hadi Pale Utakapokuwa Na Sababu Za Msingi
Za Kutokumwamini. Na Hata Unapokuwa Umelithibitisha Jambo, Endelea Kuwa
Katika Uhalisia Wako.
6. Kuacha Hobi, Marafiki
Mahusiano Ya Kimapenzi Mara Nyingi
Huhusisha Kila Mmoja Kuacha Baadhi Ya Mambo Yake Kwa Ajili Ya Mwenzake.
Hata Hivyo, Lengo Ni Kuweka Tu Uwiano Wa Mahitaji, Si Kuacha Kila Kitu
Ulichokuwa Nacho Kwa Ajili Ya Mwenzako, Ama Kwa Shinikizo, Au Kwa Kulewa
Penzi.
Iwapo Utabaini Kuwa Marafiki Zako Sasa
Wamekuwa Ni Marafiki Zako Wa Zamani Na Hobi Zako Zimebaki Tu Katika
Kumbukumbu Japo Kwa Hakika Bado Unahisi Mapenzi Katika Hobi Hizo, Basi
Tambua Kuwa Huyo Mrembo Wako Amekunywesha Sumu Ya Penzi Na Sasa Huwezi
Hata Kuitumia Vema Mantiki Yako.
Mbaya Zaidi, Iwapo Utabaini Kuwa
Marafiki Zako Wapya Ni Marafiki Wa Siku Zote Wa Mpenzi Wako Na Hobi Zako
Ni Zile Za Mpenzi Wako, Basi Tambua Kuwa Huna Tena Nafsi Yako, Bali
Umejisalimisha Mzima Mzima Kwa Mpenzi Wako. Lakini Msemo Mmoja Wa Hekima
Unatwambia Usiweke Mayai Yako Yote Kwenye Kikapu Kimoja. Yamkini
Unaelewa.
7. Kukubali Kupelekeshwa
Pengine Unakumbuka Kuwa Kuna Nyakati
Ambapo Ulikuwa Na Uwezo Wa Kujikita Katika Jambo Moja Na Kulifanya Kwa
Umakini, Huku Ukiwa Pia Mwerevu, Mjanja Na Unayejisimamia, Lakini Leo
Unayeyuka Kirahisi Tu Kama Barafu Iliyowekwa Juani! Hii Ni Hatari Kwa
Mustakabali Wa Maisha Yako.
Mbaya Zaidi Ni Pale Utakapoiacha Kazi
Yako Inayokulipa Vizuri Na Kufanya Kazi Nyingine Kwa Ajili Ya
Kumfurahisha Mpenzi Wako. Ukifika Hali Hii Ujue Wewe Mwenyewe Kuwa Hapo
Hakuna Mwanamume.
8. Utayari Wa Kufa Kwa Ajili Yake
Umewahi Kujisikia Kuwa Na Utayari Wa Kufa
Kwa Ajili Ya Mpenzi Wako? Kama Jibu Ni “Ndiyo”, Basi Fahamu Kwa Hakika
Kuwa Hayo Uliyo Nayo Si Mapenzi Bali Ni Upumbavu. Pengine Huku Ndiko
Kunywesha Sumu Ya Mapenzi. Kwa Hakika, Hakuna Mwanamke Ambaye Anastahili
Kumfanya Mwanamume Yeyote Kufa Kwa Ajili Yake.
Yamkini Wanaume Wanaolengwa Katika
Makala Haya Si Wavulana Wanaosoma Sekondari, Waliobalehe Majuzi, Ambao
Wakipenda Au Kupendwa Hujiona Kama Wako Katika Sayari Yao. Mwanamume
Aliyepevuka Hujiamini Na Hayaweki Maisha Yake Yote Mikononi Mwa
Mwanamke, Hata Kama Mwanamke Huyo Angekuwa Ndiye Mrembo Wa Dunia.
Iwapo, Ama Kwa Ujinga Au Kwa Kufahamu
Umewahi Kumwambia Mpenzi Wako: “Ukiniacha Nitajiua,” Na Ukawa Unaamini
Hivyo Kabisa, Basi Yamkini Unahitaji Kutafuta Msaada Wa Ushauri Nasaha,
Maana Kwa Hakika Umepotoka.
9. Muda Wote Unawasiliana Naye
Vijana Wa Siku Hizi Ni Watumiaji Wazuri
Sana Wa Simu, Lakini Iwapo Utabaini Kuwa Asilimia Kubwa Ya Muda Wako
Unautumia Ama Kwa Kuongea Au Kuwasiliana Kwa Ujumbe Mfupi Na Mpenzi
Wako, Basi Fahamu Kuwa Kuna Tatizo Ambalo Linahitaji Ufumbuzi Wa Haraka.
Kumbuka Kuwa Mapenzi Hayachukui Nafasi
Ya Kila Kitu. Yamkini Huyo Mpenzi Wako Amekukuta Unaishi Na Kuna Mambo
Ya Muhimu Ya Kufanya. Hebu Achana Na Simu Kwanza Ufanye Mambo Ya Muhimu
Kuhusiana Na Maisha Yako. Kama Mpenzi Wako Hakwelewi Katika Hili Basi
Hakufai.
10. Ndugu Zake Wanakufuatilia
Iwapo Utabaini Kuwa Marafiki, Ndugu Na
Jamaa Za Mpenzi Wako Wanamtonya Mpenzi Wako Kuhusiana Na Kile
Wanachokiita Mwenendo Wako Mbaya, Usipuuze Hali Hii. Kuna Uwezekano
Mkubwa Kuwa Watu Hawa Wanayo Sababu Ya Kuwa Na Wasiwasi Na Mwenendo
Wako, Kwa Hiyo Jichunguze Na Kuangalia Jinsi Unavyoenenda.
Hata Hivyo, Jambo Hili Si Ishara Njema
Ya Mustakabali Mwema Wa Uhusiano Wenu. Iwapo Mpenzi Wako Ataweka Watu
Wake Wakufuatilie, Maana Yake Halisi Ni Kwamba Hakuamini. Katika Hali
Kama Hii, Haitarajiwi Kuwa Mustakabali Wa Uhusiano Wenu Utakuwa Mzuri,
Kwani Kutakuwa Na Uingilizi Mwingi Wa Ndugu, Jamaa Na Marafiki Zake.
Unaweza Kukubali Kuendelea Kuishi Katika Hali Hii Kwa Kisingizio Cha
Mapenzi, Lakini Ukweli Ni Kwamba Hayatakuwa Mapenzi
Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
xxxxxxxxxxxxx
0 comments:
Chapisha Maoni