Licha ya mwenyewe kukanusha vikali lakini madai mazito yanasema kuwa, nyota wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ametimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi iliyopo Kunduchi-Beach jijini Dar baada ya kukosana na mwanamke anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake ambaye pia ndiye mmiliki wa mjengo huo.
Kwa mujibu wa gazeti la Risasi, pamoja na Kiba
kuendelea kusisitiza kwamba si kweli, mwanamke huyo anayeishi nchini
Singapore, aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kusoma kwenye mitandao
ya kijamii na vyombo vingine vya habari kuwa, kwa sasa Kiba anatoka na
Miss Tanzania namba 2, 2006, Jokate Mwegelo "Kidoti" huku Kiba mwenyewe
akikataa madai hayo.
"Ali (Kiba) ametimuliwa kule Kunduchi-Beach
kwenye ile nyumba aliyowekwa na yule demu mwenye fedha zake na ndiye
aliyekuwa akimgharamia kila kitu.
"Aliyemponza ni yule Kidoti, Jokate Mwegelo. Jokate amekuwa akimposti
Kiba kwenye mitandao ya kijamii, ndipo mwanadada huyo alipoona akachukia
na kumuona Kiba ameshindwa kuthamini fadhila zake," kilidai chanzo cha gazeti hilo.
Sasa hivi amerudi kwa mama yake, Kariakoo (Dar) kutokana na yeye
mwenyewe kulikoroga kwa kuupiga teke mgodi wa fedha.
"Japokuwa mara kwa
mara Kiba mwenyewe amekuwa akikanusha kujihusisha kimapenzi na Jokate,
lakini ukweli ni kwamba ameshaharibu kwa mwanadada aliyekuwa
anamuwezesha," kiliongeza chanzo hicho.
Katika kuweka sawa mzani wa madai hayo, mwandishi alimtafuta staa huyo wa Ngoma ya Chekecha Cheketua kwa njia ya simu na
kumuuliza kuhusu madai hayo na kutaka kujua anakoishi hivi sasa, ambapo
alifunguka hivi:
"Unataka kujua naishi wapi ili iweje? Wakati unajua kabisa kuna
matatizo yalinipata (kuvamiwa). Sasa nikisema si naweza kujitafutia
matatizo mengine?
"Siwezi kusema ninapoishi kwa usalama wa maisha yangu na kuhusu huyo mwanamke ni maneno ya watu wenye lengo la kunichafua.
"Jokate ni mwanamke ambaye nipo naye karibu katika vitu vingine
ambavyo ni vya msingi zaidi na si hivyo ambavyo watu wanahisi. Lakini
kama kuna mtu atahisi tofauti itakuwa juu yake. Mimi na Jokate ni
washkaji ‘long time’ (muda mrefu) katika mambo kibao.
"Kuhusu nyumba nilishawahi kufafanua kwamba siyo yangu. Kuna mtu
aliniweka kwa makubaliano maalum, lakini ninashangaa kusikia taarifa
ambazo zipo tofauti juu ya ukweli ambao mimi ninaufahamu."
Chanzo: Gazeti la Risasi/Gpl
0 comments:
Chapisha Maoni