JUMLA ya wahamiaji haramu 250 kutoka nchini Ethiopia wapo katika magereza mbalimbali nchini.
Taarifa
hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira
Silima wakati akijibu swali la Mbunge wa Koani, Amina Andrew Clement.
Katika
swali lake Mbunge huyo alitaka kujua idadi ya wahamiaji haramu kutoka
Ethiopia walioko katika magereza nchini na hatua zinazochukuliwa dhidi
yao wakishamaliza vifungo vyao.
Silima
alisema katika Mkoa wa Kilimanjaro wapo wahamiaji 68, Lindi 34, Tanga
70, Mbeya 22, Morogoro 39, Mwanza 1, Pwani 4 na Mara 12.
“Hatua
zinachukuliwa na Serikali kudhibiti wahamiaji haramu ikiwemo kuimarisha
udhibiti, kuwashitaki na kuwarejesha makwao. Hatua zinazochukuliwa na
Serikali baada ya wahamiaji haramu kumaliza vifungo au adhabu zao
walizopewa na mahakama ni kuwaondosha nchini,” alisema.
Alisema
urejeshaji wa wahamiaji haramu kutoka Ethiopia hufanyika kwa kutumia
usafiri wa ndege kwa kuwa wameacha kutumia usafiri wa barabara kutokana
na hofu ya kiusalama inayosababishwa na vitendo vya kigaidi.
Alisema
hadi sasa jumla ya wahamiaji haramu 96 wamemaliza vifungo vyao kati yao
wanaotoka Ethiopia wapo 91 na kwamba wanasubiri usafiri ili warejeshwe
makwao.
0 comments:
Chapisha Maoni