KIKAO
cha Kamati ya Ushauri cha Wilaya ya Mbeya, jana kilikaa na kupitia
mapendekezo ya kuyagawa majimbo mawili ya Mbeya na kuwa majimbo manne ya
uchaguzi kwa mwaka 2015.
Kikao hicho kiliwahusisha madiwani, wanasiasa, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na vyombo vya habari.
Katika
kikao hicho, wajumbe walikubaliana kuyagawa majimbo hayo ambayo ni
Jimbo la Mbeya Mjini linaloongozwa na Joseph Mbilinyi (Chadema). Kwa
mujibu wa mapendekezo, jimbo hilo litagawanywa na kuwa na majimbo ya
Iyunga na Sisimba.
Mapendekezo
hayo yanataka Jimbo la Iyunga liundwe na kata zote 21 za Tarafa ya
Iyunga ambayo ina jumla ya wakazi wapatao 327,122.
Jimbo la Sisimba, litakuwa na kata 15 zilizopo Tarafa ya Sisimba yenye wakazi wanaokadiriwa kuwa 106,264.
Pamoja
na idadi ya watu, vigezo vingine vilivyotumika kuyagawa majimbo hayo ni
pamoja na jiografia ya tarafa hizo kwa kuwa Tarafa ya Sisimba
imezungukwa na milima na mabonde.
Kwa
upande wa Halmashauri ya Mbeya, mapendekezo yaliyopo ni kugawa Jimbo la
Mbeya Vijijini linaloongozwa na Mchungaji Lacksoni Mwanjale (CCM).
Mapendekezo yaliyopo yanataka jimbo hilo ligawanywe ili lipatikane Jimbo la Mbeya na Jimbo la Isangati.
Jimbo
la Mbeya, litaundwa na kata 11 za Tembela, Inyala, Itewe, Njombe,
Maendeleo, Igoma, Ilungu, Ihango, Lwanjilo, Ulenje na Swaya zenye wakazi
107,349.
Jimbo
la Isangati litakuwa na kata 15 za Masoko, Ilembo, Izyira, Iwiji,
Isuto, Bonde la Songwe, Iwindi, Igale, Santiliya, Iyunga Mapinduzi,
Itawa, Utengule Usongwe na Nsalala zenye wakazi 221,480.
Akizungumza
baada ya kufungua kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyirembe
Munasa, alisema mgawanyo wa majimbo hayo umepita katika vikao mbalimbali
vya kisheria.
0 comments:
Chapisha Maoni