MKAZI
wa Mbezi Juu David Oturo, amesema yupo katika maandalizi ya
kuwasafirisha watoto wake wawili waliopoteza maisha Mei 17 mwaka huu
baada ya kupigwa shoti ya Umeme katika Kanisa la Ufufuo na Uzima
lililopo katika Viwanja vya Tanganyika Peakas Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na jana baba mzazi wa watoto hao Oturo alisema kuwa anatarajia
kuwasafirisha watoto wake ambao ni Sarah David(10) na Goodluck David(04)
leo au kesho kuelekea Mkoani Musoma kwa ajili ya mazishi.
Alisema
kifo cha watoto wake ni cha utata kutokana na kwamba watoto walikuwa ni
wengi katika eneo hilo lakini ameshangaa watoto wake wote wawili
kupigwa na shoti ya umeme na wote baada ya hapo walipelekwa katika
Hospitali ya TMJ na kuhamishiwa katika Hospitali ya Mwananyamala lakini
wote walipoteza maisha.
Akizungumzia
suala la ushiriki wa kanisa katika msiba huo alisema kuwa Askofu
Gwajima pamoja na waumini wake wanafika nyumbani kwake lakini
hawajashiriki kitu chochote.
“Kwa
sasa nipo katika maandalizi ya kuwasafirisha watoto wangu kwenda Musoma
kwa ajili ya mazishi, ingawaje katika maandalizi yangu Askofu Gwajima
na waumini wake hawajatoa kitu chochote kwa ajili yamaandalizi ya safari
hii.
“Mimi
ninachong’ang’ana ni kuhakikisha kuwa wanangu ninawasafirisha kwenda
kuwapumnzisha nyumbani kwetu nilipozaliwa ambako ni Musoma na si
vinginevyo,” alisema Oturo.
Kwa
upande wake Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima
alipotafutwa kuzungumzia swala hilo simu yake iliita bila kupokelewa na
wakati mwingine ilikuwa ilikuwa haipatikani kabisa.
Pamoja
na jitihada za kupiga simu kwa askofu huyo kugongwa mwamba, lakini
ilisikika miito ya nyimbo pamoja na mahubiri mbalimbali katika simu
yake.
Moja ya muito huo ulisikika ukisema “Biblia
ni njia kwa waliopotea, Biblia ni njia kwa waliokata tama, Biblia ni
uponyaji kwa wagonjwa, Bibilia ni faraja kwa walio na dhiki,” yalisikika maneno hayo.
0 comments:
Chapisha Maoni