SADIO Mane, raia wa Senegal amefunga magoli matatu peke yake
‘Hat-tric’ Southampton ikishinda 6-1 dhidi ya Aston Villa katika mechi
ya mapema ya ligi kuu England leo.
Mane alifunga magoli hayo katika
dakika ya 13′ 14′ na 16 hivyo kuvunja rekodi ya hat trick iliyokuwa
inashikiliwa na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Robbie
Fowler aliyefunga mabao matatu ndani ya dakika tano.
Rekodi hiyo ya Fowler imeendelea kudumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka nane (8).
Magoli mengine ya Southampton
anayochezea mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Victor Wanyama
yamefungwa na Shane Long katika dakika ya 26′ na 38′ na Graziano Pelle
alifunga goli la sita dakika ya 81.
Christiani Benteke aliifungia Aston Villa goli la kufutia machozi katika dakika ya 45′.
0 comments:
Chapisha Maoni