WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amewataka Watanzania wajiandikishe kwa wingi katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Amesema
kwamba, kama watafanikiwa kufanya hivyo, watakuwa na sifa za kuwachagua
wagombea wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25, mwaka
huu.
Waziri
Mkuu Pinda aliyasema hayo juzi alipokuwa akizungumza baada ya
kujiandikisha kwenye ofisi ya Ofisa Mtendaji wa Kata iliyopo Kijiji cha
Kibaoni, wilayani Mpanda, Mkoa wa Katavi.
“Ninawasihi
Watanzania wote tusiache kutumia fursa hii, kila mtu ahakikishe
anajiandikisha kwa sababu ni fursa pekee itakayohakikisha kila mwananchi
anashiriki uchaguzi wa kumpata rais, mbunge na diwani katika eneo lake.
“Binafsi
nimefarijika kwa kazi inayoendelea hasa hasa katika Halmashauri za
Nsimbo na Mlele ambazo zimefanikiwa kuandikisha watu kwa zaidi ya
asilimia 100,” alisema Waziri Mkuu Pinda.
Awali
akiwasilisha taarifa ya uandikishaji katika Halmashauri ya Mlele,
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Godwin Benne, alisema walilenga
kuandikisha watu 19,482 lakini hadi kufikia jana walifanikiwa
kuandikisha watu 20,292 sawa na asilimia 105.
“Kata
ya Kibaoni ambayo ina vituo sita, jana peke yake tuliandikisha watu
1,007 kikiwamo kituo cha Kibaoni ambacho Waziri Mkuu Pinda
amejiandikisha,” alisema.
Alivitaja
vituo vingine, kuwa ni Milumba, Sungusungu, Ilalangulu, Manga na Shule
ya Msingi Kakuni ambako Mama Tunu Pinda alijiandikisha juzi hiyo hiyo.
Naye,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Neneka Rashid, alisema
uandikidhaji ulianza Mei 18, mwaka huu kwenye kata 12.
Alisema
kwamba hadi kufikia juzi, kata nne zilikuwa zimeandikisha watu 12,001
ambazo ni sawa na asilimia 108.9 ingawa matarajio yao yalikuwa ni
kuandikisha watu 11,014.
0 comments:
Chapisha Maoni