Kwenye maswali na majibu ndani ya Kikao cha Bunge kibachoendelea Dodoma kuna vingi vinatokea, sasa hivi ni mijadala ya Bunge la Bajeti lakini ikifika wakati wa maswali na majibu kuna ishu nyingine huwa zinaibuliwa humohumo.. Leo niliinasa hii ya mashindano ya Miss Tanzania, kumbe kuna Wabunge hata hawayataki mashindano hayo kabisa !!
“Mimi sioni
haja ya mashindano ya mamiss Tanzania.. Sisi tunaongozwa na maadili,
unamuona mtoto wako anaenda kushindana mamiss, na ipo Kitaifa kabisa
Mheshimiwa Fenela? Unamuona mtoto anavyodhalilishwa kwa
sababu ya gari.. Jamani kama hamna gari bora mpande baiskeli au mpande
pikipiki majumbani mwenu“>>>Mbunge Faida Mohamed Bakari.
“Sisi
wazazi hasa wanawake hatutaki.. Serikali inashadadia umiss hasa mimi
nasema huu umiss una faida gani katika nchi yetu? Mbona hawafanyi na
wanaume?“>>> Faida Mohamed Bakari.
“Pamoja na
yale mapungufu ambayo ameyagusia miss Tanzania ni suala la kisanii na
yale mapungufu yalifanyiwa kazi na tukaruhusu Miss Tanzania ikaendelea“>>> Fenela Mukangala.
Ikafika time ya maswali kujibiwa >>> “Miss
Tanzania inatengeneza ajira kwa warembo na pia inatangaza nchi na
vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi na pia inatoa burudani na elimu.
Tunao warembo wenye akili nzuri wanaotumia nafasi ya Miss Tanzania
kutengeneza ajira kwa vijana wengine“>>> Waziri Fenela Mukangala.
Iko hapa sauti, ukiplay utasikiliza swali la Mbunge huyo na jibu la Waziri ilivyokuwa Bunggeni Dodoma.
0 comments:
Chapisha Maoni