Si jambo la kawaida kusikia mtoto kamuua
mama yake ama mama kamuua mtoto wake, japo kwa miaka ya sasa matukio
kama hayo yameshamiri kwa kiasi kikubwa sehemu mbalimbali duniani.
Tukio la mtoto kumuua mama yake leo limechukua headlines huko Zimbabwe baada ya kutokoea kutoelewana baina yao.
Kilichotokea ni kwamba binti wa miaka 17
alimuua mama yake kwa kumchoma moto baada kulazimishwa kufua nguo
chafu, kitendo kilichomkasirisha na kufikia uamuzi huo.
Kabla ya kumuua mama yake kwa kumwagia
mafuta kisha kumchoma moto, mama yake alimpiga kitendo kilichomuuzi
binti huyo na kufanya uamuzi huo mgumu.
Polisi wamemfungulia mtoto huyo mashtaka ya mauaji licha ya kupewa taarifa kuwa alikua akisumbuliwa na ugonjwa wa akili.
0 comments:
Chapisha Maoni