Mbunge
wa Urambo (CCM), Margaret Sitta ameishauri Serikali kuunda chombo huru
cha kusimamia elimu nchini ili kuondoa utaratibu uliopo sasa ambapo
Serikali ndio msimamizi wa shule zake na shule binafsi.
Akizungumza
jana Aprili 30, 2018 wakati akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2018/19, Margaret ambaye alikuwa
waziri wa wizara hiyo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu katika
Serikali ya Awamu ya Nne, amesema chombo hicho kitasaidia kuweka usawa
katika elimu.
“Lazima
kuwe na chombo maalum cha kusimamia elimu kwa kuchambua sera, lugha za
kufundishia kama ni sahihi ama si sahihi, kusimamia mitihani inayotungwa
je iendelee kama ilivyo na kutazama mazingira ya shule,” alisema
Margaret.
Bajeti
ya wizara hiyo ya Sh1.4trilioni imewasilishwa jana asubuhi, wabunge
wengi walioijadili waligusia kuanzishwa kwa chombo hicho, baadhi
wakibainisha kuwa Serikali imekuwa ikizikandamiza shule binafsi badala
ya kuziboresha wakati ikijulikana wazi kuwa shule hizo kwa sasa
zinafanya vizuri zaidi kuliko za Serikali.
Margaret pia ameitaka Serikali kuanzisha vyuo zaidi vya maendeleo na ufundi ili vijana zaidi waweze kupata elimu na kujiajiri.
0 comments:
Chapisha Maoni