Mahakama
ya Wilaya ya Arumeru imetishia kuifuta kesi inayomkabili Mkurugenzi wa
Shule ya Lucky Vicent na wenzake kwa sababu ya upande wa mashtaka kuomba
kesi hiyo iahirishwe mara kwa mara.
Hayo
yamesemwa na Hakimu wa mahakama hiyo, Desderi Kamugisha baada ya wakili
wa serikali, Alice Mtenga kuomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe
nyingine ili waifanyie mabadiliko hati ya mashtaka.
Kesi hiyo ilitarajiwa kuanza kusikilizwa kwa siku tatu mfululizo kwa mashahidi wa upande wa mashtaka.
Wakili
wa utetezi, Method Kimomogolo alikubaliana na hoja za wakili wa
serikali, kwamba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine.
Hakimu
Kamugisha alikubaliana na ombi la ahirisho la kesi hiyo, huku akiuonya
upande wa mashtaka kwamba kama haujajipanga vizuri kuhusu kesi hiyo
anaweza kuifuta kwa sababu inaahirishwa mara kwa mara.
Baada ya kusema hayo aliahirisha kesi hiyo hadi leo May 8, 2018 kwa ajili ya kusikilizwa kwa mashahidi wa upande wa mashtaka.
0 comments:
Chapisha Maoni