Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Wizara
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezindua mfumo
mpya wa TEHAMA kwa vituo vya kutolea huduma za afya ikiwa na lengo la
kuboresha utoaji wa huduma za afya katika vituo vyote hapa nchini.
Uzinduzi
huo umefanywa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee
na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo, Jijini Dodoma ambapo pia
alizindua kanuni za sheria ya uongozi wa hospitali za watu binafsi,
mwongozo wa viwango vya msingi kwa vituo vya kutolea huduma za afya
nchini pamoja uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri wa hospitali za watu
binafsi.
“Nina
uhakika maombi ya usajili wa vituo vya afya sasa yataenda kwa haraka.
Waombaji watajaza fomu na kulipia hukohuko walipo bila kufika ofisini
na vile vile watakuwa na uwezo wa kutumia mfumo kwa kutumia simu zao,”
alisema Dkt. Ndugulile.
Amesema
Sekta ya Afya ni miongoni mwa sekta muhimu katika Serikali ya Awamu ya
Tano ambapo sekta hiyo ni ya tatu kwa kupata bajeti kubwa. Aidha kwa
mwaka huu wa fedha jumla ya vituo vya afya 208 vimeboreshwa kwa ajili
ya kutoa huduma ya dharura ya mama na mtoto.
Dkt.
Ndugulile amesema ndani ya bajeti hii vituo vya afya 67 vitajengwa
nchini pamoja na hospitali za rufaa kwa mikoa ambayo haina hospitali za
rufaa.
Wakati
huo huo, Waziri Ndugulile ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima wa Afya
(NHIF) kufanya majukumu iliyopewa ikiwa ni pamoja kusajili vituo vyenye
uwezo wa kutoa huduma kutokana na vigezo vilivyowekwa na mfuko huo na
kuziachia mamlaka nyingine majukumu yake ya kukagua vituo hivyo kama
vile mikataba ya kazi ya wafanyakazi wa vituo husika.
Aidha
ameutaka mfuko huo kutafakari juu ya masharti yaliyowekwa katika
kusajili vituo ambapo kituo hakiwezi kusajiliwa mpaka kiwe katika
uangalizi na mfuko huo kwa miaka isiyopungua mitano.
Naye,
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Otilia Gowele amesema kanuni mpya
za sheria ya uongozi wa hospitali za watu binafsi zitasaidia kusogeza
huduma kwa wananchi pia hospitali hizo kutoa huduma kulingana na
mahitaji ya sasa.
0 comments:
Chapisha Maoni