Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo
Waziri
wa wizara ya kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu Mkuu wa
Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kusitisha mkataba wa kazi wa
Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndg Hassan Jarufo.
Waziri
Tizeba ametoa agizo hilo kwa katibu mkuu wa wizara hiyo Jumamosi 21
Aprili 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
mjini Dodoma ikiwa ni muda mchache mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya
uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa.
Akielezea
sababu za kuagiza kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo, Mhe. Dkt
Tizeba alisema kuwa hayo yamejili baada ya kuangalia mwenendo wa Ndg
Jarufo na kutafakari jinsi zao la korosho linavyoendeshwa, ikiwa ni
pamoja na kutoridhishwa na upatikanaji wa viuwatilifu kwa wakati.
Aidha,
Mkataba huo umesitishwa kuanzia leo tarehe 21 Aprili 2018 hivyo Katibu
Mkuu wa wizara hiyo atapaswa kufanya taratibu zote za kiutumishi ikiwa
ni pamoja na kumpatia taarifa haraka muhusika na utekelezaji wake kuanza
haraka.
Alisema
ndani ya muda mfupi Wizara ya kilimo itamtangaza Kaimu Mkurugenzi wa
Bodi hiyo ili kuchukua nafasi hiyo kuendeleza kusimamia sekta hiyo.
“Hizi
hatua tunazochukua ni kuhakikisha kuwa wadau wakubwa wa korosho ambao
ni wakulima wanaendelea kunufaika na zao lao, hivyo wakulima wasiwe na
wasiwasi kwani pamoja na kuondolewa Mkurugenzi huyo lakini shughuli za
serikali zitaendelea kama kawaida na maslahi yao yatasimamiwa ipasavyo”
Alikaririwa Mhe. Dkt Tizeba


0 comments:
Chapisha Maoni