Mahakama
ya Wilaya ya Dodoma leo Aprili 5, 2018 imepokea taarifa ya vipimo vya
kitabibu vya Tito Machibya (Nabii Tito) ili kujua kama ana matatizo ya
akili au la.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha leo
Alhamisi Aprili 5, 2018 amesema amepokea taarifa ya kitabibu kuhusu
Nabii Tito kutoka Isanga hivyo ataipitia ili aje atoe maamuzi siku ya
April 13 mwaka huu.
“Niseme
tu kuwa nimepokea taarifa ya kitabibu kuhusu mtuhumiwa leo asubuhi
hivyo nitaipitia ili April 13, 2018 siku ya ijumaa niweze kuitolea
maamuzi,” amesema Karayemaha.
Nabii
Tito ambaye hakuweza kuhudhuria kesi yake mara mbili mfululizo leo
amefika mahakamani baada ya hakimu Karayemaha kutoa maagizo ya mtuhumiwa
huyo kufikishwa mahakamani au aletewe taarifa rasmi ya kwa nini
hafikishwi mahakamani kusikiliza kesi yake.
Februari,
2018 Nabii Tito alidai mahakamani kuwa yeye ana matatizo ya akili
yaliyosababisha kutaka kujiua na hivyo Mahakama kuamuru akafanyiwe
vipimo vya kitabibu ili kujua kama kweli mtuhumiwa huyo ana matatizo ya
akili au la.
Nabii Tito amerudishwa rumande hadi Aprili 13 kesi yake itakapotolewa uamuzi.
0 comments:
Chapisha Maoni