Spika
Job Ndugai akiongea kwa mara ya kwanza na mtangazaji Charls Hillary
tangu arejee kutoka India kwa matibabu ameongelea suala la mbunge wa
Nzega, Hussein Bashe kutoa hoja binafsi.
Amesema
pamoja na Kanuni za Bunge pia zipo Kanuni za uendeshaji wa shughuli za
Bunge kwa wabunge wa CCM kama chama tawala na zipo kama hizo kwa wabunge
wa kambi ya upinzani ambazo zote ni sehemu ya uendeshaji wa shughuli za
Bunge.
Amesema
Bashe kama mbunge wa CCM, kanuni za wabunge wa CCM zinamtaka aipeleke
hoja yake kwenye chama chake kwanza, ikajadiliwe huko na ikikubaliwa
Bunge liweze kuipokea.
Ndugai
amesema Bunge bado halijapokea hoja hiyo kutoka kwa Bashe pia
halijapokea taarifa kutoka kwa katibu wa wabunge wa CCM kama wameipokea
hoja hiyo na wameshaurianaje.
Kuhusu afya yake, amesema imeimarika ukilinganisha na miezi michache nyuma.
Hivi
karibuni Mbunge Hussein Bashe (Nzega - CCM) alisema amemuandikia barua
Katibu wa Bunge kuhusu ombi la kuwasilisha hoja binafsi bungeni ya
kutaka kuundwa tume teule itakayochunguza matukio ya kihalifu nchini.
==>Msikilize hapo chini akiongea
0 comments:
Chapisha Maoni