Ikiwa
leo ni Kumbukumbu ya Kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine aliyefariki dunia Aprili
12, 1984 kwa ajali ya gari, eneo la Dakawa nje Kidogo ya Mji wa
Morogoro, Rais Dkt. John Magufuli amefunguka na kueleza alivyomfahamu
kiongozi huyo enzi za uhai wake na mchango wake katika Taifa letu.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Magufuli amesema;
“Katika
siku kama ya leo tarehe 12 Aprili 1984 nikiwa Mpwapwa JKT nikitumikia
jeshi langu “Oparesheni Nguvukazi” tukatangaziwa kifo cha marehemu
Edward Moringe Sokoine, ilikuwa siku ya majonzi shujaa huyu niliyemjua
na kumshabikia ikawa siku yake ya mwisho.
“Wakati
tunapoazimisha siku kama hii ya kifo chake, watanzania tuige mfano wake
kwani alikuwa msema kweli, asiyeogopa, mpiga vita rushwa,ufisadi,
unyonyaji,mzalendo wa kweli na aliyechukia rasilimali za watanzania
kuibwa.
“Marehem
Sokoine hatasahaulika katika historia ya Tanzania, ni wito wangu kwa
watanzania tumuige na kumuishi. Ni rai yangu pia tumuenzi kwa kujenga
umoja wetu , kupiga vita rushwa na kuchapa kazi . Mungu aiweke roho ya
marehemu Edward Moringe Sokoine mahala pema peponi,” amesema Magufuli.





0 comments:
Chapisha Maoni