Rais
wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Dk Akinumwi Adesina ni miongoni
mwa wageni wa kimataifa walioalikwa kuhudhuria maadhimisho ya miaka 54
ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 2018.
Mbali na sherehe hizo, rais huyo aliyewasili nchini Aprili 25, 2018 atakuwa nchini kwa ziara ya siku tatu.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) alipokewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.
Dk
Adesina ameahidi ndani ya miaka miwili ijayo, AfDB itawekeza Tanzania
zaidi ya Dola 1.5 bilioni za Marekani (zaidi ya Sh3.36 trilioni).
"Tuna
uhusiano wa muda mrefu na Tanzania ambayo ni mnufaika anayeongoza
kupata ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu Afrika. Tangu mwaka 1971,
AfDB imewekeza zaidi ya Dola 3.6 bilioni," amesema Dk Adesina katika
taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha kwa vyombo vya habari.
Benki
hiyo imefadhili mradi wa kusafirisha umeme wenye msogo wa kilovolti 400
wenye urefu wa kilomita 670 unaohusisha vituo vya kupozea umeme katika
mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga kwa Dola 220 milioni.
AfDB pia inasaidia kutekeleza Mpango wa Kukuza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (Sagcot).
Waziri
Mpango amesema AfDB ni mshirika mkubwa wa maendeleo na licha ya
kufadhili ujenzi wa barabara na nishati mwaka jana pekee ilitoa mkopo
nafuu wa Dola 50 milioni kukuza mtaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB).
Dk Adeseina atatembelea mradi wa kupooza umeme uliopo Zuzu mkoani Dodoma.
0 comments:
Chapisha Maoni