Ikiwa
ni siku moja tangu msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ azikwe, mtoto wake
wa pekee Sania Sabri ameondoka na baba yake kurudi jijini Dar es Salaam.
Marehemu
Masogange alizikwa jana Aprili 23 mwaka huu pembeni mwa nyumba ya baba
yake, Gerald Waya katika kijiji cha Utengule, Mbalizi II mkoani Mbeya.
Baba
wa marehemu, Waya amesema mjukuu wake, Sania ameondoka leo Aprili 24 na
baba yake Sabri Athman kuelekea jijini Dar es Salaam, ili kuwahi
masomo kwa kuwa sasa hakuna shughuli yoyote ya familia.
Amesema
licha ya kumfahamu mjukuu wake Sania, hakuwahi kumfahamu baba yake
hivyo msiba huo ndiyo uliowakutanisha na kufahamiana kwa mara ya
kwanza.
“Mjukuu
wangu Sania ameondoka leo alfajiri na baba yake. Sababu ni kuwahi
masomo shuleni kwani tumeona shughuli zote ziliisha jana hakuna sababu
ya kuendelea kuwa naye hapa, atakuja wakati wa kumaliza matanga,”
amesema.
Waya
amesema shughuli za kuondoa matanga zitafanyika baada ya siku 40 kupita
na jana walifanya shughuli ya kuwaaga waombolezaji waliolala msibani
hapo na kubakia familia tu.
“Hivi
sasa kama unavyoona hakuna kinachoendelea, tumebaki familia tu ambayo
tutaendelea kuomboleza hadi baada ya siku 40 ya matanga. Haitafanyikia
hapa nyumbani badala yake tutarudi kule nyumbani asili ambako ndiko kuna
makaburi ya ukoo na nyumba ya baba yangu ipo kule,” amesema Waya.
Amesema
familia zao zote huzikwa kwenye makaburi hayo, lakini mtoto wake
ameamua azikwe pembezoni mwa nyumba yake ili asikae mbali naye. Pia,
kwenye makaburi ya pamoja kwa sasa hapapitiki kwa urahisi kutokana na
mvua zinazoendelea.
0 comments:
Chapisha Maoni