Kamati
Kuu ya chama hicho jana Jumatano, Mach 28 ilikutana na kutoa msimamo
wake ambapo walidai kuwa hawapo tayari kuendelea kuonewa.
Juzi Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman
Mbowe na viongozi wenzake walifikishwa mahakamani na kuswekwa rumande
baada ya kunyimwa dhamana,
Baadhi
ya viongozi wa Chadema waliozungumza ni pamoja na Makamu mwenyekiti wa
Chadema, Profesa Safari, Godbless Lema na John Mrema, ambapo mkutano huo
pia ulihudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Kuu akiwemo Edward Lowassa,
Fredrick Sumaye na Meya Boniface Jacob.
Makamu
Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Abdallah Safari alisema tukio la
kunyimwa dhamana na kupelekwa rumande kwa viongozi hao ni uonevu kwani
dhamana ni haki ya mtuhumiwa anapokamatwa.
“Licha
yaa jitihada za mawakili wetu kuwatetea viongozi wetu lakini
wamewanyima dhamana. Tumemwandikia barua Jaji Mkuu kumwambia mbona kila
tunapokamatwa linapofika swala la dhamana tunakataliwa? Jaji Mkuu kajibu
kirahisi sana eti kateni rufaa,” alisema Prof. Abdallah Safari.
Kwa
upande wake, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema kwamba
anafahamu kuwa upo mkakati wa kuwafunga Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,
Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine waliowekwa mahabusu tangu jana.
“Huo
mchezo wanaotaka kufanya waendelee nao, wamewanyima dhamana ili kesi
iendeshwe haraka na wawafunge kama alivyofanyiwa Sugu. Tunajua vikao
vyao na nia yao. Wakitaka tusema, ukiogopa kufa utakufa.
“Sisi
tutaweka mambo mengi hadharani, sina uhakika kama Mwenyekiti wetu
kesho(leo) atapewa dhamana. Hapa tulipofika hatuwezi kuendelea kuishi
kwa hofu. Hii vita si ya Chadema, hii ni vita ya demokrasia, Akwilina
hakuwa mwanachama wa Chadema lakini aliawa, sasa nafikiri inatosha.
“Baada
ya kutoka mahakamani kesho(leo) tutakutana na kuamua iwapo tufungulie
maji na tuanike kila kitu kwa sababu hatuna namna. Yeyote aliyehusika
tutamuanika,” alisema Lema.
0 comments:
Chapisha Maoni