Mahakama
Kuu nchini Kenya imewataka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Waziri wa
Mambo ya Ndani na Kamishna wa Uhamiaji kufika mahakamani leo kujitetea
kwanini wasifungwe jela au kulipa faini kwa kuidharau Mahakama.
Jaji
wa Mahakama Kuu, George Odunga alisema kuwa maafisa hao wakuu
Serikalini walifanya kosa la kuidharau mahakama kwa kukataa wito wa
kumfikisha mahakamani hapo mwanasheria Miguna Miguna, Jumatano wiki hii.
Jaji huyo amesema kuwa Mahakama haiwezi kuchezewa na Serikali na haitaruhusu hilo lifanyike kwani ndicho chombo cha haki.
Miguna
alishikiliwa na Polisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo
Kenyatta alipojaribu kurejea nchini humo akitokea nchini Canada
alikopelekwa kwa nguvu kwa madai ya kutokuwa raia wa Kenya.
Serikali
inadai Miguna aliyekuwa anatuhumiwa kwa uhalifu wa kushiriki zoezi la
kumuapisha Raila Odinga kama ‘Rais wa Watu’, alipinga uraia wake mwaka
1988, madai ambayo mwanasheria huyo ameyapinga. Miguna anadai ni raia wa
kuzaliwa wa Kenya mwenye uraia pia wa Canada lakini hajawahi kuukana
uraia wa nchi hiyo kama inavyodaiwa.
Hata
hivyo, mbali na tishio hilo la Mahakama kwa viongozi hao wa vyombo vya
usalama, jana usiku Miguna alisafirishwa bila hiari yake hadi Dubai.
Mahakama imewahi kuamuru Muguna aachiwe huru na kama kuna madai yoyote anapaswa kufikishwa mahakamani na sio vinginevyo.
0 comments:
Chapisha Maoni