Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mmiliki wa IPTL, Harbinder Sethi
akatibiwe katika Hospital ya Taifa Muhimbili baada ya mshtakiwa huyo
kulalamika afya yake imearibika sana.
Mbali
ya Sethi, mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara James Rugemarila ambapo
kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha
fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Bilioni
309.
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi leo March 28, 2018 kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na pia wanafatilia vielelezo vya upelelezi nje ya nchi.
Baada
ya kueleza hayo, Seth alisimama na kumueleza Hakimu Shaidi kuwa; 'Afya
yangu imearibika sana, nahitaji kupelekwa hospitali.'
Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Shaidi amesema ni dhahiri afya ya mshtakiwa ikiangaliwa hata kwa macho inaonekana ni dhahifu.
“Naamuru
mshtakiwa akatibiwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ili afya yake
iwe njema,” amesema Hakimu Shaidi na kuahirisha kesi hiyo hadi April
11,2018.
Washtakiwa
wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi,
kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za kimarekani
22, 198,544.60 na Sh, bilion 309.
0 comments:
Chapisha Maoni