Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewaunganisha
marafiki waliogeuka kuwa mahasimu wakubwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Fm, Ruge
Mutahaba.
Rais Magufuli amewaunganisha wawili hao leo kabla ya kuhitimisha hotuba yake jijini Tanga kuhusu uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi jijini humo.
Baada ya kumuomba muda mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ili afanye kitu tofauti, Rais Magufuli aliwaita jukwaani Makonda na Ruge na kuwataka wamalize tofauti zao.
“Nimewaleta vijana wote ninawapenda na wao nataka wapendane,” alisema Rais Magufuli.
“Haya shikaneni mikono hapa. Nataka mambo yenu ninyi wawili yaishe. Nataka mfanye kazi kwa ajili ya Tanzania. Nakupongeza Ruge kwa nyimbo nzuri na Mungu awabariki sana,” aliwaeleza. kauli hiyo ikisababisha wananchi kulipuka kwa shangwe.
Makonda na Ruge waliingia katika mtafaruku baada ya Clouds Media Group kudai kuwa mkuu huyo wa mkoa alivamia katika studio zake usiku akiwa na askari wenye silaha na kulazimisha kipindi kisichokidhi sifa za kitaaluma za uandishi wa habari kurushwa kupitia kipindi cha Shilawadu kwa maslahi binafsi.
Kutokana na kitendo hicho, Kamati Maalum iliyoundwa na aliyekuwa waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni, Nape Nnauye kiliwasilisha ripoti yake na kudai kuwa ni kweli tukio hilo lilitokea.
Kufuatia ripoti hiyo, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) lilitangaza kumfungia Makonda kutangazwa au kuchapishwa na chombo chochote cha habari ambacho ni mwanachama wa Jukwaa hilo.

0 comments:
Chapisha Maoni