Mkuu wa Wilaya ya Ilemela , Dk Leonard Masale, ameachia ngazi baada ya kufikisha umri wa kustaafu.
Akithibitisha
taarifa hizo mchana wa leo Julai 5, Dk Masala amesema hayuko ofisini
tangu Julai Mosi baada ya kufikia umri wa miaka 60, ambao ni wa kustaafu
kwa lazima kwa mtumishi wa umma.
Amesema
hivi sasa nafasi yake inakaimiwa na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Khadija
Nyembo, na yeye tayari amepokea mafao yake ya kustaafu kutoka mfuko wa
Pensheni kwa Watumishi wa Umma, PSPF, baada ya kuwaandikia barua
kuwajulisha kuhusiana na kustaafu kwake miezi sita iliyopita.
Hata
hivyo, kiongozi huyo amesema yuko tayari kulitumikia taifa katika
nafasi yoyote atakayopewa iwapo atahitajika kwani hajachoka nabado ana
uwezo wa kufanya kazi.
0 comments:
Chapisha Maoni