Mkuu
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Wilaya (OCCID), Yustino Mgonja
ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa alimkamata Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu
(ZCO), Camilius Wambura kumtaka afanye hivyo.
Mgonja
ambaye ni shahidi wa nne katika kesi ya kutumia lugha ya uchochezi
inayomkabili Lissu, alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey
Mwambapa kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.
Akiongozwa
na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi, shahidi huyo
alidai kuwa Juni 28, mwaka jana, Wambura alimpa maelekezo ya kumkamata
Lissu kwa kosa la kutoa lugha za uchochezi katika viwanja vya mahakama
hiyo.
Alidai
kuwa Juni 29 mwaka jana saa 7 mchana alienda nyumbani kwa Lissu maeneo
ya Tegeta wilayani Kinondoni, ambapo alimkamata na kumfikisha katika
ofisi ya ZCO na kumkabidhi.
“Nilipewa
amri na ZCO nikukamate hivyo kwa mamlaka hayo bila kuwa na hati ya
ukamataji naweza kukukamata; kwani makosa yoyote ya jinai unaruhusiwa
kukamata bila kuwa na hati hiyo,” alidai Mhonja.
Pia
alidai kuwa kumpinga Rais anapokosea sio kosa na kwamba tafsiri ya
maneno aliyoyatoa, ndio yamesababisha kukamatwa na kushitakiwa kwa
kutumia lugha za kichochezi.
Katika
mashitaka yake, Lissu anadaiwa kuwa Juni 28, mwaka huu akiwa katika
viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alitoa kauli za uchochezi
kuwa “Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidikteta uchwara inahitaji
kupingwa na kila Mtanzania kwa nguvu zote, ‘huyu diktekta uchwara lazima
apingwe kila sehemu’. Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi
inaingia ndani ya giza nene.’’
0 comments:
Chapisha Maoni