Naibu
Meya wa Jiji la Arusha, Viola Likindikoki, pamoja na madiwani wengine
wawili wa Chadema wamekamatwa jana na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa
sababu ambazo mpaka sasa hazijafahamika.
Meya
wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro amesema Viola pamoja na madiwani hao
wawili walikamatwa jana Alhamisi wakiwa katika mkutano wa ndani
uliokuwa ukisikiliza kero za wananchi.
“Nipo
Tanga kikazi na nilimkaimisha nafasi yangu Viola, kwa kawaida Alhamisi
tunasikiliza kero za wananchi, wakati wakiendelea kusikiliza kero ndipo
walipokamatwa,” alisema.
Wengine
waliokamatwa katika tukio hilo ni diwani wa viti maalumu (Chadema),
Kata ya Ngarenaro Happiness Charles na diwani wa Viti Maalumu kata ya
Olorieni, Sabrina Francis.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo amesema kwa kifupi kwamba jeshi lake linawashikilia kwa uchunguzi.
Diwani
wa viti maalumu (Chadema), Jenipher Lomayan amesema madiwani hao
walikamatwa jana saa 9 alasiri wakiwa ndani ya ofisi ya Meya wa Jiji
la Arusha wakisikiliza kero za wananchi.
Lomayan,
amesema wakiwa ndani ya ofisi hizo polisi waliovalia nguo za kiraia
waliingia na kuwaeleza kwamba wako chini ya ulinzi na wanatakiwa kufika
mbele ya makao maku ya jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi.
“Wale
polisi walitaka kuichukua simu ya Naibu Meya na ndipo madiwani wawili
(Sabrina na Happiness) wanaoshikiliwa waliingilia kati na kuwazuia
polisi wasimnyanganye simu hiyo na ndipo na wao wakaunganishwa katika
tukio hilo,” amesema.
0 comments:
Chapisha Maoni