Hawa ni Baadhi ya Wanawake Wajane walioshiriki katika hafla ya Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq, jana Kigogo-Post Dar es salaam. |
Mwenyekiti
Msaidizi wa Chama cha Wajne Tanzania Wilaya ya Ubungo Dar es salaam Mh
Josephine Chale amemtaka Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dr.John Magufuli kuwaangalia Wajane kwa jicho la pili ili aone namnagani
anaweza kuwasaidia katika Nyanja ya sheria ambayo itazuia wajane
kuonewa kwa kudhulumiwa haki zao
Chale
amewaomba Wajane nchini wasijisikie wakiwa, kwani kuwa Mjane haina
maana ndio mwisho wa Maisha,kwani haliya kuwa maisha yanaendelea
Aidha
Chale ameushukuru Uongozi wa Msjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq
kuweza kuwaalika Wajane katika futari ya pamoja ili Wajane wajisikie
kwamba na wenyewe wanatakiwa katika jamii, ili wasijitenge kama vile
kwamba wamefiwa basi ndio maisha yamefika mwisho.
Hayo
alisema jana katika halfa ya futari ya pamoja na Wajane,iliyoandaliwa
na Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq Vilivyopo Kigogo
Post Dar es salaam.
“Napenda
tena kuwashukuru Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq kwa
kutualika sisi wajane, tumepata faraja kubwa sana, kwani na sisi
tutaenda kufanya kama wanaofanya wenzetu ili tuwape amani
wajane.Tunashukuru sana sana,tunamuomba Mungu awape Moyo wa upendo,
awape riziki na awape maisha marefu.”
Kwa
upande wake Mtumishi wa Imam Swadiq Bi.Zaynab Ndete alisema lengo la
hafla hii ya Futari ya Pamoja na Wajane, ni Tumewaalika wanawake Wajane
kutoka Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Dar es salaam, lengo kubwa ni
kuzungumza nao na kuwapatia muongozo wa Kisheria, hususani zinazowahusu
wao baada ya kufiwa na waume zao.
“Kwa
kweli swala ya Ujane ni swala zito ni swala gumu, kwasababu ni swala
linalomuhusu mwanamke, kama tunavyoangalia katika jamii yetu ya
Kitanzania wajane wengi wanapokuwa wametoza wame zao, wanakuwa ni watu
ambao wanakuwa katika matatizo makubwa sana, miongoni mwa matatizo
wanayokumbananayo ni kutengwa au kunyanyapaliwa na familia ya mume
,kunyang’anywa haki zao za msingi, kunyang’anywa mali zao ambazo
wameachiwa kama urithi na wame zao” alisema Ndete
“Sisi
Uongozi wa Masjid Ghadir na Chuo cha Imam Swadiq tumewaita hapa kwanza
kuwasaidia waweze kuzifahamu haki zao, wamama wajane hawatakiwi wawe
wanyonge pale wanapoondokewa na wame zao,kuondokewa na mume ni jambo
Mwenyezimungu (swt) ameliandika kuwa ni lalazima kwani anaweza kuondoka
Mume au Mke” aliongeza Ndete.
“Dini
ya Kiislam imesimama kidete juu ya kuwatetea wanawake wajane, kwani
ukiwa mjane unahaki ya Kuishi kama wengine,anahaki ya kuwa na
mali,unahaki ya kuwa Kiongozi,unahaki ya kuwa Bosi, anahaki kuwana amani
na upendo, anahaki ya kuwa Muajiriwa, anahaki ya kuolewa na Mwanaume
mwingine,anahaki ya kumiliki” alisisitiza
Hatahivyo
Mtumishi Ndete aliwaomba Wanawake wajane wasiwe wanyonge na wasimame
kidete kuweza kusimamia malezi ya familia zao kwani jukumu la kuwalea
watoto aliokuwachia mumewe iko mikononi mwako.
0 comments:
Chapisha Maoni