Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 31 Mei, 2017 amefanya uteuzi wa Naibu Magavana wawili wa Benki
Kuu ya Tanzania (BOT).
Mhe.
Rais Magufuli amemteua Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Naibu Gavana
anayeshughulikia Uchumi na Fedha (Economic and Financial Policies –
EFP).
Kabla
ya uteuzi huu Dkt. Yamungu Kayandabila alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazina anachukua nafasi iliyoachwa na
Dkt. Natu E. Mwamba ambaye amemaliza muda wake.
Mhe.
Rais Magufuli amemteua Dkt. Bernard Yohana Kibese kuwa Naibu Gavana
anayeshughulikia Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha (Financial
Stability and Deepening – FSD).
Kabla
ya Uteuzi huo Dkt. Bernard Yohana Kibese alikuwa ni Mtaalamu wa Uchumi
na Fedha wa BOT na anachukua nafasi iliyoachwa na Lila H. Mkila ambaye
amemaliza muda wake.
Uteuzi huu unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
31 Mei, 2017
0 comments:
Chapisha Maoni