Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mh. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli amewapandisha vyeo Maafisa watano wa Magereza kuwa
Naibu Makamishna na wengine 24 kuwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi
wa Magereza kuanzia tarehe 25 mwezi Mei, 2017.
Waliopandishwa
vyeo kuwa Naibu Kamishna wa Magereza ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza Uwesu H. Ngarama, Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza, Dar es
Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon M. D. Nkana,
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Dar es Salaam, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Jeremiah .M.C. Nkondo, Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza
Tusekile S. Mwaisabila, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi pamoja na
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Augustine S. Mboje ambaye ni
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam.
Waliopandishwa
vyeo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza ni Kamishna Msaidizi
wa Magereza Mbaraka Sultan Semwanza, Mwalimu wa Hisabati na Kemia shule
ya Sekondari Bwawani inayosimamiwa na Jeshi Magereza, Kamishna Msaidizi
wa Magereza George Togholai Mwambashi, Mkuu wa Kitengo cha Sheria Makao
Makuu ya Magereza Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Charles
R. Novat, Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo Makao Makuu ya Magereza Dar es
Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Faustine Martin Kasike Mkufunzi
Mwandamizi Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) Kunduchi Dar es Salaam.
Wengine
ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Joel Silverster Bukuku, Mdhibiti wa
Shirika la Magereza, Kamishna Msaidizi wa Magereza Deogratius Ndaboine
Lwanga, Afisa Mnadhimu, Magereza Makao Makuu Ukonga, Dar es Salaam,
Kamishna Msaidizi wa Magereza Boyd Patric Mwambingu, Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Magereza Athuman Ambayuu Kitiku,
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Magereza Hassan
Bakari Mkwiche, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi
wa Magereza Luhende DAVID Makwaia, Mkufunzi Mkuu wa Mafunzo ya Kijeshi
na Msaidizi wa Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira Mbeya, Kamishna Msaidizi
wa Magereza Hamza Rajab Hamza, Afisa Mnadhimu wa Magereza Mkoa wa
Tabora na Kamishna Msaidizi wa Magereza Jeremiah Yoram Katungu, Msaidizi
Ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Magereza Makao Makuu Dar es Salaam.
Wengine
ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Mzee Ramadhan Nyamka, Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza Afwilile Mwakijungu,
Mkuu wa Gereza Isupilo Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Magereza
Ally Abdallah S. Kaherewa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Ruvuma, Kamishna
Msaidizi wa Magereza Salum Omar Hassan, Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa
Singida, Kamishna Msaidizi wa Magereza Ismail T. Mlawa, Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Magereza Chacha Bina Jackson,
Mdhibiti wa Fedha Makao Makuu ya Magereza Dar es Salaam na Kamishna
Msaidizi wa Magereza Rajab Nyange Bakari, Mkuu wa Kikosi Maalum cha
Kuzuia Ghasia Magereza Ukonga Dar es Salaam.
Wengine
ni Kamishna Msaidizi wa Magereza Kijida Paul Mwankingi, Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Magereza Julius Cosmas
Ntambala, Msimamizi Mkuu wa Ujenzi wa Nyumba 320 za Kuishi Askari Gereza
la Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza Mussa Musuluzya Kaswaka, Afisa
Mkaguzi Makao Makuu Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza
Justine M. Kaziulaya, Mratibu Msaidizi Baraza la Usalama la Taifa na
Kamishna Msaidizi wa Magereza Bertha Joseph Minde ambaye ni Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Manyara.
Imetolewa na
Meja Jenerali Projest Rwegasira
Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
6 Juni 2017
0 comments:
Chapisha Maoni