"Si
kweli kuwa sivai sare cha CHADEMA, hata nilipokuwa CCM nilikuwa nashona
shati la rangi moja ama kijani au njano kisha naweka nembo maalumu ya
chama, vivyo hivyo hata CHADEMA naweka nembo maalum.
"Na jambo kubwa hapa ni kuwa, nisihukumiwe kwa kuvaa au kutokuvaa sare za CHADEMA lakini kwa matendo yangu."
Hayo
ni maneno yaliyotolewa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Ngoyai Lowassa alipokuwa akijibu swali
la mtangazaji wa kituo cha Azam Tv, Charles Hillary aliyetaka kujua
kwanini havai sare za CHADEMA katika matukio mbalimbali kama ilivyokuwa
CCM.
Lowassa
alienda mbali na kusema kuwa, sare si jambo kubwa sana kwani mtu
anaweza kuvaa sare na bado akawa si mmoja wenu. Unaweza kukuta mtu kavaa
nguo za kijani lakini kiukweli moyoni si wa CCM
Aidha,
Lowassa alisema, alipomaliza Chuo Kikuu alikwenda jeshini na kwa muda
wote huo alikuwa akivaa magwanda, hivyo alishavaa vya kutosha, na umri
wake kwa sasa si wa kuvaa tena.
Alipoulizwa
kama uamuzi wa kutokuvaa sare ni mbinu ya mwaka 2020 aweze kupata
kuungwa mkono na wanachama wa CCM na CHADEMA, alicheka kisha akasema
kuwa, kama ni mbinu basi anaamini itafanyakazi.
0 comments:
Chapisha Maoni