test

Jumatatu, 5 Juni 2017

Kauli ya Zitto Kabwe Baada ya Mwenyekiti Wa Chama Chake Kuteuliwa Kuwa Mkuu wa Mkoa


Nimekuwa naulizwa Sana kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama chetu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. 
Nimekuwa kimya Kwa sababu tumepokea Taarifa za uteuzi kutoka katika vyombo vya Habari. Mwenyekiti yuko nje ya nchi na kutokana na tofauti za masaa bado hatujawasiliana nae. Tutatoa tamko kamili atakapokuwa amerejea nchini.

Ninawataka wanachama wote wa Act Wazalendo wawe watulivu na Kama kuna masuala yanayohusu maamuzi ya vikao vya Chama tutawajulisha.

Aliyeteuliwa ni Mwenyekiti wa Chama Taifa, sio mshauri au mwanachama tu. Ni mmoja wa viongozi wa juu wa Chama chetu. Uteuzi wake unahitaji kikao cha Kamati Kuu ya Chama kukaa na kujadili. Nitaweza kutoa Taarifa baada ya vikao vya Kamati Kuu ya Chama. 
Kwa sasa umma usubiri vikao Kwa mujibu wa Katiba ya Chama chetu.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni