Mkuu
wa utumishi Jeshi la Wananchi Tanazania (JWTZ), Meja Jenerali Harrison
Masebo amekanusha taarifa zinazoenea mitandaoni kuhusu kutangazwa kwa
nafasi za ajira na kwamba watu wanaotangaza hivyo ni matapeli waepukwe.
Meja
Jenerali Masebo amebainisha hayo baada ya kuenea uvumi mitandaoni na
mitaani kwa baadhi ya watu kujifanya wanahusika na jeshi hilo katika
idara ya kutoa ajira kwa wananchi.
"Kumekuwa
na vikundi ama watu ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa
wakijitangaza wao wanauwezo kutoa ajira, vikundi hivyo msivisikilize
siyo vikundi rasmi ama watu hao siyo rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi
nasema kuanzia leo mtu akisiikia kuna mtu anamfuata anamwambia kuna
nafasi ya kujiunga na mafunzo ya JKT ajue huyo mtu siyo halali ni muongo
na tapeli" -alisema Meja Jenerali Masebo.
Pamoja
na Hayo Meja Jenerali Masebo amesema mara zote Jeshi limekuwa likitoa
ufafanuzi kuhusiana na masuala ya ajira lakini wanashangazwa na kundi
hilo namna wanavyofanya kutaka kupitia 'shortcut'.
"Jeshi
limekuwa likifafanua mara kwa mara kuhusu taratibu za kujiunga nafasi
za mafunzo JKT na taratibu za kujiunga na jeshi la wananchi lakini
katika mazingira ambayo tunashindwa kuyaelewa hawa watu au vikundi ndiyo
wamekuwa wajanja kiasi cha kuwarubuni vijana, wazazi na wazazi
wakaamini kwamba zipo njia mbadala za kujiunga 'shortcut' napenda kusema
hakuna shortcut hapa" - alisisitiza Meja Jenerali Masebo
Pamoja na hayo, Meja Jenerali Masebo aliendelea kufafanua baadhi ya mambo kwa kusema
"Kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama hata wakiwa Uhamiaji, Zima
moto, Magereza, Polisi, TANAPA na Jeshi lenyewe ukitaka kujiunga na
Jeshi la Wananchi maana yake ni kwamba kuna utaratibu maalumu ambapo
kwanza kuna kikao ambacho wenyekiti wa kikao hicho ni mimi Mkuu wa
Utumishi Jeshini kwa hiyo vyombo vingine vya ulinzi na usalama vinaleta
wawakilishi ambao ni maofisa watumishi tunakaa pamoja kila taasisi,
wanaleta idadi ya watu wanaowahitaji" - Meja Jenerali Masebo aliongeza.
0 comments:
Chapisha Maoni