Serikali imesema haitaruhusu usafirishaji wa madini moja kwa moja kutoka mgodini na kupelekwa nje ya nchi.
Hayo
yameelezwa leo Alhamisi na Waziri wa Fedha na Mipango, Phillip Mpango
wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti kwa mwaka 2017/18.
Badala
yake kutakuwa na viwanja maalumu vya kimataifa katika bandari, migodini
na madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali kabla ya kusafirishwa
nje.
“Kibali hicho kitatozwa ada ya asilimia moja ya thamani ya madini hayo,” amesema.
Amesema Serikali itatangaza rasmi tarehe rasmi ya kuanza kwa ada hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni