Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema
kuwa Serikali itaenzi michango yote ya wasanii wakongwe hapa nchini.
Ameyasema
hayo kufuatia kifo cha mzee aliyebuni nembo ya taifa, Mzee Francis
Kanyasu maarufu kwa jina la ‘Ngosha’ aliyekuwa amelazwa katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili kwaajili ya kupatiwa matibabu.
“Tutaendelea
kuwa karibu na familia ya marehemu Mzee Francis Kanyasu, kwani
katuachia alama kubwa sana na mchango wake katika Taifa utakumbukwa
milele”, amesema Dkt. Mwakyembe.
Hata
hivyo, katika kushiriki msiba huo, Mwakyembe atawakilishwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Godfrey
Mngereza ambapo atakuwa akiiwakilisha Serikali.
0 comments:
Chapisha Maoni