Mbunge Joseph Kasheku maarufu kama Musukuma amewaponda mawaziri
waliotumbuliwa na Magufuli Nape Nnauye na Charles Kitwanga kwa kuiponda
serikali baada ya kutolewa kwenye uwaziri na kumtaka waziri wa elimu
ahakiki vyeti vyao.
Amemshangaa Kitwanga kwa kusema sasa ameondoka kwenye uwaziri na ataanza
kuisema serikali akiuliza kwenye baraza la mawaziri wanaambiwa nini.
Amemponda kauli ya kitwanga ya ku mobilize wananchi 10,000 kuharibu mtambo wa maji na kuhoji vyeti vyake vipi?
Kuhusu kauli ya Nape kusema CCM haitarudishwa endapo haitatekeleza
bajeti ya maji amesema sio kwdeli kwa kuwa miaka mingi hawatekelezi
ilani na wanachaguliwa na wananchi hawawategemei kwa maji tu na bado
muda upo
Pia amesema hela ya bajeti ya maji ni nyingi iwapo itatoka yote. amesema
bajeti liyopita ilipangwa kutolewa bilioni 915 lakini mpaka leo ni 181
tu ndio imetoka