Kupungua
kwa bei za hisa za kampuni ya ACACIA kwa asilimia 32.7, na UCHUMI 28.6%
na JHL 17.8% kumetajwa kuwa sababu ya kupungua kwa ukubwa wa mtaji wa
kampuni zilizoorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa
Sh. Trilioni 1.5 kutoka Shilingi Trilioni 19.9 wiki iliyopita hadi
Shilingi Trilioni 18.4 wiki iliyoishia tarehe 26 Mei 2017.
Wakati
akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Miradi na Masoko wa DSE
Patrick Mususa, pia alisema mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia
Mei 26, 2017 yamepungua kutoka thamani ya Sh. Bilioni 29.5 wiki
iliyopita hadi Shilingi Bilioni 2.9, kutokana na mauzo ya hati fungani 7
za serikali zenye thamani ya bilioni 3.8 kwa jumla ya gharama ya
bilioni 2.9.
kwa upande wa viashiria,Mususa alisema
“Kiashiria cha kampuni zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI
kimepungua kwa pointi 171 kutoka pointi 2,288 hadi pointi 2,117 kutokana
na kupungua kwa bei za hisa za kampuni mbali mbali zilizopo sokoni.
Wakati Kiashiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimeongezeka kwa pointi 6
kutoka pointi 3,357 wiki iliyopita hadi pointi 3,363 wiki hii.”
“Sekta
ya viwanda imeendelea kubaki kwenye pointi 4,228 wiki hii. Sekta ya
huduma za kibenki na kifedha wiki hii imeongezeka kwa pointi 17 kutoka
pointi 2,551 hadi pointi 2,568 kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa za
CRDB kwa asilimia 2.7%.Sekta ya huduma za kibiashara wiki hii
imeendelea kubaki kwenye pointi 2,969,” alisema.
Pia, Mususa alisema thamani ya mauzo ya hisa imepungua kutoka Sh. Bilioni 8 wiki iliyopita hadi Shilingi Bilioni 2.6 wiki hii.
Hata
hivyo, Mususa alieleza kuwa, idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa
imeongezeka kutoka hisa Milioni 1.1 hadi hisa Milioni 2.2, hali
kadhalika mtaji wa kampuni za ndani umeongezeka kwa Bilioni 13 kutoka
Shilingi Trilioni 7.056 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 7.069 wiki
hii. kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa za CRDB (2.7%).
0 comments:
Chapisha Maoni