KATIBU
mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi amefunga kozi ya
utawala bora iliyoendeshwa na mkufunzi wa FIFA Henry Tandau iliyokuw
ainafanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam
Kozi
hiyo inayosimamiwa na Kamati ya Olimpiki ilianza Mei 08 na kufungwa Mei
12 huku kukiwa na washiriki 15 kutoka klabu mbali mbali za ligi kuu na
taasisi za michezo.
Akizungumza
wakati wa kufunga kozi hiyo Bayi amesema kuwa hii ni kwa mara ya kwanza
kwa wawakilishi kutoka klabu mbalimbali za Ligi Kuu kushiriki katika
mafunzo haya ambayo ni muhimu sana kwa maendeleo ya michezo nchini.
Amesema
kuwa, ana imani kubwa sana kuwa elimu hii waliyoipata wataenda kuitumia
vizuri katika kuziendesha klabu zao na kuzieletea maendeleo kwani
msingi mkubwa wa maendeleo ya soka ni kuwa na utawala bora.
"Elimu
hii mliyoipata leo nina imani kubwa sana mtaitumia vizuri kwani wengi
wenu mnatoka katika klabu za Simba, Yanga na Azam na maendeleo ya mpira
wa miguu yanaletwa na utawala bora na wasiende kuweka vyeti ndani bali
wanatakiwa kuvitumia kwa ajili ya manufaa ya vizazi vijavyo,"amesema
Bayi.
Mkufunzi
wa FIFA Henry Tandau amemshukuru Bayi kwa kuweza kukubali kuwa mgeni
rasmi kaika mafunzo hayo na kumuahidi kuwa elimu hii waliyoipata
wanaimani kuwa washiriki wote wataenda kuelimisha na wengine na kuleta
utawala bora kwenye klabu zao.
Mafunzo
hayo ya siku 5 yameratibiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini huku
ikiwa ni kwa mara ya kwanza tofauti na miaka mingine kufanyika mikoani
pia yameweza kuleta tija kwa washiriki kufahamu mambo mbalimbali
yanayohusu michezo ikiwemo riadha.
Katibu
mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akizungumza wakati
wa kufunga kozi wa mafunzo ya utawala bora iliyoendesha na Shirikisho
la Mpia wa Miguu (FIFA) kupitia kamati ya Olimpiki iliyoanza Mei 08
mpaka Mei 12 Jijini Dar es salaam.
Mkufunzi
wa FIFA Henry Tandau akizungumza wakati wa kufunga kozi wa mafunzo ya
utawala bora iliyoendesha na Shirikisho la Mpia wa Miguu (FIFA) kupitia
kamati ya Olimpiki iliyoanza Mei 08 mpaka Mei 12 Jijini Dar es salaam.
Kulia ni Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi.
Katibu
mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha
mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka Kituo cha JKM Park Kassim
Liogope mafunzo yaliyomaliza leo Jijini Dar es salaam.
Katibu
mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha
mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka klabu ya Yangaa ambaye ni
afisa masoko na mratibu wa matawi Omari Kaya mafunzo yaliyomalizaleo
Jijini Dar es salaam.
Katibu
mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha
mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka Azam Saad Kawemba ambaye ni
Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo mafunzo yaliyomalizika leo Jijini Dar es
salaam.
Katibu
mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha
mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu
Nchini Wilfred Kidau katika mafunzo yaliyomalizika leo Jijini Dar es
salaam.
Katibu
mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha
mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka Klabu ya Simba Said Tuli
ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa Simba mafunzo yaliyomalizika
leo Jijini Dar es salaam.
Katibu
mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha
mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka bodi ya ligi Fatma Abdala
mafunzo yaliyomalizika leo Jijini Dar es salaam.
Katibu
mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akiw akatika picha
ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya utawala bora yaliyomalizika leo
Jijini Dar es salaam.Picha na Zainab Nyamka.