Serikali
imevifuta vituo vyote vya taasisi zisizo za kiserikali vinavyotoa
huduma za afya ya VVU na Ukimwi, kwa makundi maalum kutokana na
kubainika kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja.
Baada
ya kuvifuta, serikali imeelekeza huduma hizo sasa kutolewa tu kwenye
vituo vya umma pamoja na vituo vya afya vya binafsi vilivyosajiliwa.
Tamko
hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ambapo amesema kuwa
serikali imefikia uamuzi huo kutokana na maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa
makundi maalum kuongezeka ikilinganishwa na wastani wa kiwango cha
maambukizi nchi nzima.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu Prof. Muhammad Bakari Kambi amesema katazo hilo
limelenga kupunguza maambukizi ya VVU na Ukimwi ambayo kwa sasa
yameongezeka.
Wakati
huo huo Waziri Ummy Mwalimu amewataka Watanzania kubadilisha kadi za
homa ya manjano za zamani na kupatiwa kadi mpya na kusisitiza kuwa
kuanzia tarehe 31 Machi mwaka huu kadi za zamani za homa ya manjano
hazitatumika na kueleza gharama ya kubadilisha ni Shilingi 500 kwa
Mtanzania na dola 10 kwa raia wa nje.