Habari zilizonifikia hivi punde toka kwa Mtumishi mmoja anayefanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi ni kuwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg. Ngalinda Hawamu Ahmada amefariki dunia ghafla usiku wa tarehe 30/11/2016.
Habari zaidi zinasema kuwa Mkurugenzi huyo aliyezaliwa kati ya mwaka 1983/4 alianza kulalamika kuwa anajisikia vibaya akiwa ofisini ambapo baadaye alimpigia simu Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) ambaye alikuja na Ambulance na kumpeleka hospitali ambako aliaga dunia.
Huyu ni moja ya Wakurugenzi wapya walioteuliwa na Mh. Rais mwezi Julai mwaka huu.CHANZO JAMII FORUM