Jana,
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, ilishindwa kusikiliza maombi ya
kuongezewa muda wa kuwasilisha notisi ya kukata rufaa ya kupinga kuzuiwa
kwa dhamana ya Lema.
Mawakili wa Serikali waliomba muda wa kuwasilisha hoja za kupinga maombi hayo.
Maombi
hayo, yaliyotarajiwa kusikilizwa jana na Jaji Dk Modesta Opiyo
yalikwama kutokana na kusudio la pingamizi lililowekwa na mawakili
waandamizi wa Jamhuri katika shauri hilo, Paul Kadushi na Maternus
Marandu.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya Jaji Opiyo kuahirisha kusikiliza maombi
hayo, Wakili wa Lema, Sheck Mfinanga alisema mawakili wa Serikali,
wameomba wapewe muda kuwasilisha kiapo kinzani dhidi ya maombi hayo.
Alisema
Jaji Opiyo alitumia busara kutoa uamuzi kuwa mawakili wa Jamhuri
wawasilishe hoja hizo, Desemba 13 na upande wa utetezi utazijibu siku
hiyo hiyo na uamuzi utatolewa Desemba 14, saa 6.00 mchana.
Jana Lema hakufika mahakamani, kwa kile kilichoelezwa kuchelewa kupelekewa hati ya kufikishwa mahakamani.
Lema
anaendelea kushikiliwa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kupinga
uamuzi wa hakimu mkazi, Desdery Kamugisha aliyempa dhamana Lema katika
kesi namba 440 na 441/2016 ya kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais
John Magufuli.
Lema
anatuhumiwa kuwa kati ya Oktoba 23 hadi 26, mwaka huu alitoa kauli za
uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli katika maeneo tofauti katika
mikutano yake ya hadhara.
Miongoni
mwa kauli za Lema ni: “Nchi itaingia katika machafuko kama haitafuata
misingi ya katiba na sheria na pia Rais Magufuli asipobadilika”
Lema
pia akiwa katika uwanja wa shule ya Sekondari Baraa alitoa kauli kuwa:
“Kiburi cha Rais akiendeea kujiona yeye ni Mungu, hatafika 2020, Mungu
atakuwa amechukua maisha yake, Rais ni mbabe…”