Wiki iliyopita niliishia
pale nilipokuwa nikielezea muunganiko wa Aliens na makundi ya
wanasayansi wa Marekani ambao wamekuwa wakielezwa kuwa huingia mikataba
mbalimbali ya kubadilishana teknolojia na uvumbuzi wa teknolojia mpya.
Mfano ni ile Teknolojia ya Aliens Software. SASA ENDELEA…
Katika kuchimba juu ya
viumbe hao na nikushauri msomaji wangu kuwa na utamaduni wa kujifunza
vitu vipya kila siku hasa vile ambavyo havipo kwenye utaratibu wa maisha
yetu ya kila siku, itakusaidia kujua vitu kwa manufaa yako binafsi.
Kuhusu Aliens, inaelezwa
kwamba, kwa bahati mbaya, mikataba ya wanasayansi hao wa Marekani na
Aliens huwa na masharti mengi mabaya ambayo yanamuathiri na mengine
yameshamuathiri moja kwa moja binadamu na bado inasadikiwa kuwa madhara
mengine yanakuja. Wapo wasioamini lakini wengine wanaamini huo ndiyo
ukweli.
Mwaka 1952, nchini Marekani
kuliibuka utani kuwa Aliens walitua rasmi ikulu ya nchi hiyo kwa lengo
la kuingia mikataba mbele ya rais wa wakati huo, Harry Truman. Ndivyo
umma ulivyoaminishwa na wataalam wa propaganda.
Pia kitendo cha UFO
kuonekana huko Washington, Marekani katika kipindi hichohicho, ndipo
watu wakaanza kukubaliana na uvumi uliokuwa umeenezwa kuwa Aliens, UFO
na wanasayansi wa Marekani walikuwa wana uhusiano.
Uwepo wa mawasiliano hayo
ulitikisa Marekani ikiaminika kuwa ndiyo mwanzo wa uvamizi wa viumbe hao
duniani. Usiku mmoja, mnara wa rada ya Uwanja wa Ndege wa Washington
ulinasa vifaa visivyojulikana ambavyo vilikuwa vikikatiza angani kwa
kasi ya ajabu kisha vikaelekea moja kwa moja kwenye Ikulu ya Marekani
(White House).
Wakazi wa jirani na eneo
hilo walishuhudia vitu kama baluni za rangi za njano vikidondoka kutoka
angani. Vitu hivyo vilikuwa na mikia. Muda mfupi baadaye rubani mmoja
alishuhudia UFO saba zikirandaranda angani.
Baadaye anga lote lilijazwa
na vitu hivyo vilivyo-kuwa na mwanga mkali. Vitu hivyo vilishu-hudiwa
na macho ya watazamaji hivyo ule uvumi sasa ukageuka habari ya kweli.
Wakati hayo yakiendelea,
kuliibuka habari za mauaji ya kimbari huko Amerika ya Kusini. Ilielezwa
kuwa mauaji hayo ya kutisha yalifanywa na hawa Aliens. Hata hivyo,
baadaye ilisemekana kuwa shetani alikuwa ametembelea Amerika ya Kusini.
Swali ni je, watu walitambuaje kuwa ni shetani?
Ilibidi kurudi kwenye maandiko juu ya uumbaji wa mbingu na nchi ili kujua kama Mungu alimuumba shetani?
Biblia inasema kuwa Mungu
aliumba malaika wengi sana. Lusifa alipend-eza zaidi ya malaika wengine
lakini kiburi kilimwingia, akaasi. Alifanikiwa kushawishi theluthi moja
ya malaika wote na wote walifukuzwa kutoka mbinguni (shetani alianguka
kutoka mbinguni kama mwanga wa radi (Luka 10:18).
Mbingu ni dunia ya roho
(spiritual world) sayari kama Dunia, Mars, Jupiter na nyingine ni
ulimwengu wa kuonekana. Kwa kawaida binadamu hawezi kuona dunia ya roho
ila akifunguliwa macho ya roho ataona.
Hapa duniani tunaongozwa na
hisia tano tu, sight, smell, hearing, taste na touch (au feel). Hiyo
ndiyo maana binadamu anaongozwa na muda na nafasi. Kwa mfano, huwezi
ukapenya kwenye ukuta au kupaa angani kama ndege. Hebu fikiria tu kuwa
na uwezo wa kunusa au kuona sauti!
Itaendelea wiki ijayo, usikose.