test

Jumamosi, 22 Oktoba 2016

Zaidi ya milioni bado wanatumia Samsung Galaxy Note 7


Taarifa zinasema zaidi ya watu milioni bado wanaendelea kutumia simu za Galaxy note 7 licha ya kampuni ya Samsung kutaka zirejeshwe kiwandani na kubadilishiwa kwa simu zingine.


Takwimu zilizotolewa na gazeti JoongAng Daily linasema kwamba wengi
wamegoma kurudisha simu hizo kwa madai kuwa hawawezi kupata
mbadala wa simu kama hiyo kwa ubora.

Samsung walisitisha uuzaji wa simu hizo na kutaka zirejeshwe kiwandani
baada ya kuripotiwa matukio ya ulipukaji yaliyosababishwa na Battery.

Tangu Samsung kutangaza kusitisha uuzaji wa simu hizo
na bado wateja kadhaa wanaendelea kuzitumia hakuna
taarifa yoyote ya ulipukaji wa simu hizo licha ya kuendelea kutumiwa.

Kampuni ya Samsung imeanza kufanya uchunguzi wa
matukio hayo ya ulipukaji wa simu hizo.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx