test

Jumatatu, 31 Oktoba 2016

Bondia Thomas Mashali auwa kwa mapanga kwa kusingiziwa ni mwizi





image.jpeg 
Thomas Mashali,bondia mashahuri wa Tanzania amefariki usiku wa leo baada ya kupigwa mapanga maeneo ya Kimara.Inasemwa kuwa Mashali alikuwa kambini akijiandaa na pambano,lkn alitoka kambini na jamaa zake na kwenda kunywa moja moto na moja baridi.

Baada ya kupata kilaji,Mashali alihama Bar moja na kwenda nyingine,ambapo wanasema akilewa huwa anakuwa na fujo.Sasa aliingia Bar nyingine akaanza kuleta ubabe wa kupiga watu.Raia wakamuitia mwizi,watu wakaja na mapanga na marungu wakampiga mpaka kufa.Walipokuja kugundua ni Mashali,ilikuwa ameshauwawa na kupoteza damu nyingi.

Madereva wa bodaboda wakamchukua na kumpeleka Muhimbili.Mpaka sasa mabondia wanakusanyika Muhimbili kwa ajili ya utaratibu wa mazishi.

Kwa Heri Bondia Thomas Mashali.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx