Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo uliofanyika mapema leo |
- SBL yaizindua bia hiyo katika muonekano mpya
- Yashinda zaidi ya medali 10 za ubora wa kimataifa
Dar es
Salaam Oktoba 28, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza
kuanza kwa sherehe maalumu kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa
kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana
na uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.
Akizungumza jana
jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa
SBL Helene Weesie, alisema mbali na kuonesha mafanikio ya bia ya Serengeti kwa
kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru
wateja wake na umma wa Watanzania kwa kuikubali bia ya
Serengeti kama chaguo lao la hivyo kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza
hapa nchini.
“Tunawashukuru wateja
wetu, wafanya biashara, wasambazaji, mashirika ya sekta binafsi, serikali na
wadau wote ambao kimsingi wametusaidia na kuwa
nasi katika safari yetu hii ya mafaniko,” alisema Weesie.
Bia ya Serengeti Premium
Lager ni ya kwanza kutengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100hapa nchini ikiwa
ni ubunifu wa Mpishi Mkuu mtanzania aitwaye Winston Kagusa ambaye
alichanganya mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na vionjo
vya hapa nchinikupata kupata kinwaji hiki kinacopendwa na wengi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi
Mkuu, bia ya Serengeti ilizalishwa kwa mara ya kwanza ikilenga kufikia sehemu
ndogo maalumu ya soko lakini azma hii ilibadilishwa na kuzalishwa kwa wingi
kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya bidhaa hiyo jambo ambalo
lilisababisha kuanzishwa uzalishaji zaidi katika viwanda vya SBL vilivyoko
Moshi na Mwanza.
Aidha Mkurugenzi huyo
aliendelea kusema kwamba katika kipindi chote cha miongo miwili bia ya
Serengeti imekuwa na vifungashio vya muonekano tofauti tofauti vinavyoakisi
mabadiliko ya kinyakati na mahitaji ya wateja wake. “muonekano mpya
tunaouzindua leo hii ni muendelezo wa kielelezo hiki kwamba daima SBL tunajali
mahitaji ya wateja wetu na tuko karibu nao, amesema Weesie.
“Tunaona fahari
kuzalisha Bia ya Serengeti Premium Lager katika ubora
uleule wa hali ya juu katika viwanda vyote vitatu, na huu ni uthibitisho halisi
kutokana na kutambuliwa na wateja wetu wa ndani pamoja na
medali zaidi ya 10 za kutambulika
kimataifa ambazo bia hii imeshinda. Tunaahidi wateja wetu kwamba
tutaendeleakuzalisha Serengeti Premium Lager katika ubora wa hali ya
juu kwa kuzingatia vigezo vya ubora vilivyoanishwa na Shirika la
Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO),” alisema
Weesie.