Inahitajika nidhamu ya hali ya juu sana kifikra na kimaamuzi, kutoyumbishwa na habari zinazovuma kila kukicha katika taifa letu kwa sasa. Juzi UKUTA, jana kupatwa kwa jua, leo noti mpya kuchapishwa, kesho mtu kakamatwa kwa kumtukana Rais, hujakaa sawa mara wanafunzi hewa!
Ukiamua kukisemea kila kinachosikika utajitia "stress" zisizo na sababu na utapoteza uelekeo. Huu ndio wakati unaohitaji kujipambanua na kujidhibiti, kwa sababu kinyume na hapo unaweza kugeuka mbwa unaehangaishwa na mifupa inayorushwa kila siku.(tena mingine kwa makusudi kukupoteza na kutafuta huruma zako). Ndio maana kwa sasa nimeamua kutohangaika kabisa na taarifa za habari hasa za kwenye TV!
Kila siku ninashangilia maisha (huwezi kunikuta nikilalamika hata kwa bahati mbaya), kwa sababu ninajua(kwa uhakika kabisa) KWAMBA MABADILLIKO SASA YAMELIFIKIA TAIFA kwa ajili ya manufaa yangu! Full stop! Mengine wanajua wenyewe wanaohusika nayo, hayanihusu!
#SmartMind

